Facebook

Thursday 27 November 2014

Duka lawabagua wateja wazawa China.

Duka moja la nguo mjini Beijing China
limezua mjadala nchini humo baada ya
kuweka maelezo yanayopiwapiga marufuku
wateja wake raia wa Uchina.

Duka hilo limehusishwa katika mgogoro wa
ubaguzi wa rangi baada ya kuweka maelezo
yanayosema ''Raia wa Uchina
hawaruhusiwi ,isipokuwa wafanyikazi pekee
kulingana na gazeti rasmi la Beijing.

Kulingana na mfanyikazi mmoja wa duka
hilo,wateja wa kichina wanaudhi kwa kuwa
wanawake wa kichina hujaribu nguo nyingi
katika duka hilo bila kununua.
Duka hilo pia lililazimika kumlipa mteja wake
mmoja raia wa kigeni dola 5,000 baada ya
kipochi chake kuibwa huku ukanda wa video
wa CCTV ukionyesha kuwa mtenja mmoja raia
wa Uchina ndiye aliyemwibia.

Lakini mfanyikazi mwengine amesema kuwa
lengo la duka hilo haswa ni kuwazuia
washindani wake kuiga mtindo wa ngu za duka
hilo.

Maelezo hayo yamezua lalama katika mitandao
ya kijamii huku mtumiaji mmoja wa mtandao
wa Weibo akiuliza iwapo taifa hilo bado ni
Uchina ama vipi.

''Duka la aina hii ni muhimu iwapo
litafungwa'',alisema mtumiaji mwengine wa
mtandao wa Weibo.
Mwengine aliandika ''kunifanyia maeonevu
nyumbani kwangu'',alisema mtu mwingine
huku akiongezea kuwa haoni kwa nini mmiliki
wa duka hilo aliamua kulifungua nchini uchina
iwapo hawataka wateja wa Uchina.

Lakini wataalam wa sheria wameliambia gazeti
la vijana la kila siku mjini beijing kwamba huku
maelezo hayo yakiwa ya kibaguzi,mmiliki wa
duka hilo hajakiuka sheria kwa kuwa Uchina
haina sheria ya kupinga ubaguzi wa rangi.

0 comments:

Post a Comment