Facebook

Friday 21 November 2014

Polisi wazuia milango ya Bunge,Wabunge waruka ukuta kuingia ndani,mabomu ya yatumika kuwatuliza.

Spika wa Bunge
la Nchi ya Nigeria,Aminu Tambuwal amelazimika
kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo
wa dharura baada ya Polisi kufunga milango
ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.

Spika huyo alijitambulisha kwa Maafisa
Usalama hao ili wamruhusu aingie lakini
hakuna aliyeonekana kujali ombi lake wala
kumjibu, japo baadaye walimruhusu aingie
kupitia mlango mdogo wa dharura huku
wabunge wengine wakizuiwa kuingia kitendo
kilichowafanya waamue maamuzi magumu ya
kuingia ndani ya Bunge kwa kuruka ukuta.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nigeria, Suleiman
Abba amesema walilazimika kuzuia mtu
yeyote kuingia ndani ya jengo hilo na
kuweka ulinzi wa hali ya juu baada ya kupata
taarifa kwamba kuna majambazi walipanga
kuvamia Bunge hilo.

Polisi waliwashambulia kwa gesi ya machozi
Wabunge waliokaidi amri ya kutokuingia
Bungeni, Wabunge wawili walipoteza
fahamu katika vurugu hizo.

0 comments:

Post a Comment