Facebook

Wednesday 19 November 2014

Miss afariki dunia zikiwa zimebaki siku 25 kufanyika kwa shindano la Miss World.

Zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya kufanyika
kwa shindano la Miss World mwaka
2014 ,Miss Hondurus Maria Jose Alvaroe
pamoja na dada yake Sofia Trinidad Alvaroe
mwenye miaka 23 wamekutwa wamekufa
baada ya kupotea kwa siku sita.
Kwa mujibu wa kituo cha BBC tukio hilo
lilitokea alhamisi ya wiki iliyopita wakati
wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya rafiki wa
dada yake ikiwa ni siku moja kabla mrembo
huyo mwenye miaka19 hajaondoka kuelekea
jijini London tayari kwa ajili ya kushiriki
shindano hilo.

Polisi nchini humo wamesema mpaka sasa
bado hawajafahamu chanzo cha mauaji hayo
pamoja na wahusika na tukio hilo lakini
mashuhuda wanasema wasichana hao
waliondoka kwenye sherehe hiyo wakiwa na
gari ndogo ambayo halikuwa limesajiliwa.

Taarifa za kupotea kwao zilipatikana jumapili
baada ya kutorejea nyumbani huku simu zao
zikiita bila majibu.
“Siku zinakwenda bila kuwaona
wanangu,lazima polisi watakua na majibu ya
haya”alisema mama mzazi wa wasichana hao.

Miili yao ilipatikana leo asubuhi katika eneo
ambalo inasemekana walionekana kwa mara ya
mwisho wakiwa wote.

Chanzo:bbc.com

0 comments:

Post a Comment