Facebook

Friday 21 November 2014

Ronaldo akubali kuosha vyombo baada ya kufungwa.

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil
Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada
ya kushindwa katika mchezo wa karata na
mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na
kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea
dola 50,000 za hazina yake ya kutoa
msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38
alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo
kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili
hao katika meza ya pokerstar, Casino ya
Hippodrome mjini London ambapo Nadal
alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao
wawili kukutana katika chumba kimoja ni
chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi
kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo
kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha
vyombo vya Nadal alivyotumia kula.

0 comments:

Post a Comment