Facebook

Saturday 29 November 2014

LIVE:Yanayojiri Bungeni: Jumamosi, 29 Novemba 2014 (Hatma ya Sakata la Tegeta Escrow Account)



SAA 3:00 ASUBUHI
Baada ya jana bunge kuahirishwa usiku, Leo saa tatu limerejea tena na aliekalia kiti ni mama Anna Makinda na ameshaahirisha bunge mpaka saa tano asubuhi kupisha vikao vya vyama(caucus) kuketi.

SAA 5:00 ASUBUHI
 Lukuvi: Wabunge tumetumia fursa ya kukaa kwenye vyama, CCM tumekaa kwa sababu tumefanya baadhi ya marekebisho ili tutoke na maazimio, tunaomba tuendelee na majadiliano na naumba utuongezee saa moja

Mnyika: Waziri amesema consultation zinazoendelea ni za CCM hatuwezi kutoka kama bunge moja, naomba muongozo hii habari ya kuweka maazimio ya chama kwa kutumia wingi.

Lukuvi: Naomba tushauri kwa pamoja nje ya bunge na niko sawa na Mnyika.

Spika: Naagiza viongozi wa upinzani na wenzao wakae pamoja maana hatutafika na anapendekeza mpaka saa kumi

Zitto: Serikali imeomba saa moja hivyo napendekeza masaa mawili tu, saa kumi ni mbali sana.

Mbatia: Nakubaliana na hoja ya waziri, kamati ni ya bunge na sio chama. Napendekeza saa nane ili iwe masaa matatu.

Tuwashauri waende na naunga mkono hoja ya saa kumi au saa tisa

Wenje: Napendekeza consultation, kamati iende wakakubaliana na turudi saa kumi na cauvas ziwe briefed

Makinda: Nataka turudi saa kumi,

Silinde: Naungana na suala la saa kumi, lakini wote waliotumiwa kwenye ripoti wasihudhurie.

Zitto pia achukue watu wake wachache wahudhurie

Bunge limeahirishwa mpaka saa kumi


SAA 6:50 MCHANA
Kikao cha CCM kimeitishwa mchana huu baada ya mapumziko ya bunge.

Tayari makamu wa rais ameshafika na viongozi waambata wote wa CCM, kinafanyika ukumbi wa White House.

Jambo la kuhashiria kuwa huenda jioni kukawa na breaking news ni kuwa tayari gari binafsi ya waziri mkuu yenye namba za usajiri T 164 AKF aina ya range rover imeshawasili eneo hili sambamba na familia yake.

Habari zilizozagaa toka kwa wabunge hapa ni kuwa jaribio la jana la kuwatuliza wabunge wa CCM limekwama kulingana na michango ya wabunge asubuhi, Sasa wamepanga binu mbili, moja ni kushinikiza bunge liiagize serikali ifanye uchunguzi kupitia ripoti ya CAG, PCCB na mapendekezo ya PAC na kisha bunge lijalo mwakani Feb 2015 serikali ije na majibu.

Na mbinu ya pili ni kukubali yaishe watu wawajibike leo leo.  

0 comments:

Post a Comment