Facebook

Saturday 22 November 2014

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza abakwa na kujeruhiwa vibaya Mwanza.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza A
katika shule ya sekondari Ntunduru
wilayani Sengerema mkoani Mwanza
(jina limehifadhiwa, 14),
amejeruhiwa vibaya sehemu za siri
na shingoni kutokana na kukabwa
shingoni wakati akibakwa ndani ya
chumba cha darasa la shule hiyo
mchana.

Tukio hilo lilitokea Novemba 15,
mwaka huu mchana huku baadhi ya
walimu wakidaiwa kuwapo shuleni
baada ya mwanafunzi huyo kuitwa na
mhitimu wa kidato cha nne ambaye
anatuhumiwa kutenda kosa hilo.

Mwanafunzi huyo baada ya kuingia
katika darasa hilo, alikutana na
wanafunzi wawili wa kidato cha nne
waliomkaba shingo na kumziba mdomo
kisha kumvua nguo na kuanza
kumtendea ukatili huo.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Carren
Yunus, alisema watuhumiwa hao
lazima wapatikane na kuchukuliwa
hatua za kisheria.

“Pamoja kuwasaka watuhumiwa pia
lazima ufanyike uchunguzi wa kina
juu ya usalama wa wanafunzi wa kike
katika shule hii binafsi
mchanganyiko ya bweni,” alisema
Yunus.

Makamu mkuu wa shule hiyo, Bahati
Charles, alithibitisha kutokea kwa
tukio na tayari wanafanyia
uchunguzi pamoja na vyombo vya
dola.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, ni
tabia tu ya vijana wa leo kukosa
maadili,” alisema Charles.

Polisi wilayani Sengerema
imethibitisha kuwapo tukio hilo
lenye jalada Seng/RB/2949/2014 ya
Novemba 15, na kuwataja watuhumiwa
ambao hata hivyo majina yao
yanahifadhiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,
Valentino Mlolowa, alithibitisha
kutokea kwa tukio na hilo na kusema
msako wa wahusika unaendelea.

Chanzo:Nipashe

0 comments:

Post a Comment