Facebook

Thursday 20 November 2014

Rais wa Simba akana usajili wa Wachezaji wa Kigeni.

RAIS wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema
kwamba hawana nafasi ya kusajili ya
mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel
Okwi, Amisi Tambwe na Paul Kiongera
wanawatosha.

Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo
vya habari vimekuwa vikiwahusisha
washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na
Mganda Danny
Sserunkuma kusajiliwa na Simba.
Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni
mchezaji wao wa zamani, ameomba mwenyewe
kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika
hawana nafasi ya mchezaji
wa kigeni.

“Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu
yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba
hatujazungumza nao,”amesema Aveva

0 comments:

Post a Comment