Facebook

Monday 24 November 2014

CCM YATAKA WALIOHUSIKA NA SAKATA LA ESCROW KUWAJIBISHWA KISIASA NA KISHERIA.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Kinana anena

"Muda wa kuvumiliana, kubebana na kulindana umekwisha kila mtu atabeba msalaba wake. Mara unakuta hapa huyu kala (kaiba), yule mwizi anamlinda mwizi mwenzake haiwezekani tukaendesha chama na serikali hivi"

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Prof. Mtopa amesema

"Enzi za Mwalimu  suala hili lisingefika hapa lilipo kwani angekuwepo angewacharaza viboko watu wote waliohusika na Escrow pamoja na kuwafukuza kazi wote waliohusika na ufisadi huo bila kujali nani ni nani"

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye

"Ukipewa dhamana ya kuongoza nchi lazima ujipange kwenye maadili na miiko ya uongozi kwani hata rasimu ya katiba ambayo wapinzani wanaipinga bila sababu za msingi, ibara ya tano na sita zinazungumza kwa kina kuhusu maadili ya viongozi.... Sasa wakati umefika kila mtu aliyekula fedha hizo kwa namna yeyote ile atabeba mzigo wake mwenyewe, hatupo tayari kuchafuliwa kama chama kwa sababu ya watu wachache, umeshindwa kufanya kazi unaiba utasepa, uache chama chetu safi"

0 comments:

Post a Comment