Facebook

Wednesday 19 November 2014

Mwandishi mwingine wa habari afariki dunia.

Baada ya kuripoti kifo cha Mwandiashi wa habari nguli wa Gazeti la Mtanzania INNOCENT MUNYUKU.Hii ni taarifa nyingine mbaya iliyoikumba sekta ya habari nchini.

Taarifa zilizotufikia BantuTz.com hivi punde ni kwamba mwandishi mwingine wa habari Baraka Karashani amefariki dunia.Kifo hicho kinapelekea kufikisha idadi ya waandishi wahabari wawili waliofariki siku hii ya leo

Baraka Karashani ni mwandishi wa habari za michezo, aliyepata kufanya kazi katika gazeti la Dimba, Mtanzania na Bingwa,alikuwa ni mwanachana wa TASWA.

Kabla ya mauti hayajamkuta Mwishoni alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni kampuni Dar es Salaam.

Baraka Karashani Ni mtoto wa Mwanahabari nguli,aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Herald Zimbabwe, Mzee Fili Karashani.

Baraka Karashani amefia katika hospitali ya Lugalo iliyoko maeneo ya Mwenge Jijini Dar Es Salaam.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa mbalimbali kwa wakati na muda muafaka.

0 comments:

Post a Comment