Facebook

Tuesday 25 November 2014

Taarifa kutoka kwa Mh Zitto Kabwe kuhusiana na ukaguzi Maalumu akaunti ya Tegeta Escrow

Tarehe 20 Machi, 2014 Kamati ya PAC
ilimwagiza CAG kufanya Ukaguzi Maalumu
kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kufuatia
kuchotwa kwa tshs 200 bilioni kutoka Benki Kuu
ya Tanzania na kulipwa kwa kampuni ya PAP.
Mawanda ya ukaguzi ni:
Hadidu rejea

1. Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa
kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na
TANESCO.

2. Kuchunguza kama wakati escrow inafunguliwa
kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki IPTL,
kama ilikuwa imefilisiwa na kama ilikuwa
imehamisha umiliki wake kwa kampuni ya PAP.

3 Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi wa
kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar
na kumiliki IPTL

4 kuchunguza chanzo cha mgogoro kuhusu tozo
kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha
ushahidi wowote kuwa mgogoro uliamuliwa kwa
faida ya IPTL

5 kuchunguza kama ilikuwa sahihi kwa
mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi
ya VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni kutokana na
tozo ya capacity charges na TRA wachukue hatua
gani kuhakikisha kodi hiyo inakusanywa

6 kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa
kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango gani
kilikuwepo wakati IPTL wanalipwa na kiwango
gani kitapaswa kulipwa zaidi kutoka tanesco

7 kuchunguza madai ya benki ya standard
chartered kwa tanesco na madai mengine yeyote
yanayohusiana na mkataba wa kuzalisha Umeme
wa IPTL na iwapo Serikali imejihadhari na
uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa,
nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu
mikataba ya kimataifa na ya uwekezaji.

8 kuchunguza iwapo Wizara ya Nishati na
madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya
tegeta escrow ilifanya 'due diligence' ya kutosha
kabla ya kuingia makubaliano ya kutoa fedha
zilizopo akaunti ya tegeta escrow. Kupata
Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
madini ni kwa nini aliagiza ukaguzi maalum
wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye mchakato
mzima na ilhali akijua PAC tayari imeanza
mchakato wa ukaguzi.

9 kutoa mapendekezo ya njia bora za kisheria
kulinda Taifa kutoingia hasara zaidi katika
mkataba wa IPTL chini ya wamiliki wapya.

10 kutoa ushauri kwa kamati ya PAC juu ya
mapendekezo ya hatua ambazo Bunge linapaswa
kuchukua kuhusu matokeo ya ukaguzi huu
maalumu

0 comments:

Post a Comment