Facebook

Friday 21 November 2014

KUNA GHARAMA KUBWA SANA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI KUJA KUMSAFISHA MIZENGO PINDA,

Tangu mwaka 2008 kumekuwepo na vipindi vingi vya mpito kwa watanzania kupoteza imaan na watendaji wao wa serekali, hii na inatokana na mtendaji mkuu serekalini na msimamizi wa shughuli za kiserekali bungeni kukosa mwelekeo (Focus) wa kiuongozi.

Katika historia ya uongozi tangu kuanzishwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pm mizengo pinda ndiye waziri mkuu pekee aliyepoteza ushawishi na imaan kwa wananchi, taasisi za kiserekali na zisizo za kiserekali, watendaji wa serekali wanasiasa na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na vyama vya ushirika.

Kwa mujibu wa kumbukumbu katika historia ya nchii hii Pm Pinda Ndiye waziri mkuu pekee aliyepigiwa kura ya kutokuwa na Imaan naye (Vote Of No Confidence) na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano, wakiwemo wabunge wa vyama vyote ccm na upinzani...'

Mara mbili mfululizo wabunge wamekuwa na zoezi la kukusanya maoni na sign za wabunge mbali mbali ikiwa ni sehemu ya kuendesha zoezi la kumuondoa madarakani waziri mkuu Mizengo Pinda.!

Hii ni Ishara tosha sana kwa chama cha mapinduzi kuona namna waziri mkuu anayetokana na chama cha mapinduzi ameshindwa kuwa mhimili imara kama kiranja mkuu wa serekali

Ikumbukwe kwa nyakati tofauti pinda kupitia mamlaka yake au utendaji wake ameingiza serekali katika migongano, isiyo ya lazima,mikwaruzano na misuguano inayoindolea imaan serekali dhidi ya wananchi, asasi za kiraiya vyama vya wafanyakazi,watumishi wa umma, vyama vya siasa na hata raiya mmoja mmoja kukosa imaan na serekali kutokana na utendaji na uwajibikaji wa pm.!

Nchi imetitia katika migogoro ya Aridhi iliosababisha mauwaji ya wafugaji na wakulima Pm akiwepo,Nchi Imepitia vipindi vya mpito vya misuguano ya kimaslai na watumishi mbali mbali wakiwemo ma dakitari, walimu, na vyama vya wafanyakazi Pm akiwepo na kukosa majawabu (say)

Nchi Imepitia Maafa na mauwaji ya raiya wema kwa kukosa usimamizi mzuri kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu
ikumbukwe kuna unyanyasaji wa haki za raiya na uvunjwaji wa haki za kibinadamu katika operation ambazo pm kupitia ofisi yake ya waziri mkuu amekuwa akiziratibu....'
Matokeo (outcome) ya operetion kimbunga ni uwajibikaji mbovu wa ofisi ya waziri mkuu, matokeo (Outcome) ya operation Tokomeza ni uwajibikaji mbovu wa ofisi ya waziri mkuu Huku kote hakuna mahala unaweza kuacha kuihusisha Ofisi ya waziri mkuu na Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Tumefika hapa kutokana na kuwa na waziri mkuu ambaye hatoshi kiutendaji na katika uwajibikaji wake dhidi ya Mamlaka aliyonayo

Nchi imepita vipindi vingi vya mpito vilivyosababishwa na utendaji wa Waziri Mkuu, Leo nchi nzima inaimba wimbo wa ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma kwa kukosa Mtu Anayeweza kuwajibika moja kwa moja, wananchi wanalalamika, wanasiasa wanalalamika,watendaji serekalini wanalalamika, viongozi nao wanalalamika Hakuna wakutekeleza kila mtu mlalamikaji, hakuna wa kumuagiza mwinzie atekeleze hata mtendaji mkuu amekuwa na kawaida kulalamika (kulia) utekelezaji hakuna.

Hapa Hatujazungumzia Ufisadi unaotokea tamisemi na Namna operation ya ujenzi wa gesi la mtwara kuja dsm ulivyoleta machafuko ambayo waziri mkuu alikosa mamlaka dhidi ya yote hayo

Ni wakati sahihi kwa chama cha mapinduzi kuisimamia serekali yetu kuwajibika dhidi ya ufisadi mkubwa wa Escrow via Iptl

Ile dhana ya Collective Ministerial responsibility ndio wakati wa kufanya kazi

Kumekuwa na utamaduni kwa Pm kuwalazimisha watendaji waliichini yake na mawaziri wake kuwajibika na yeye akibaki salama,

Ilitokea Hivyo katika saga la Wizara ya afya kati ya serekali na madakitari ikumbukwe waziri mkuu alishindwa kufanya chochote mpaka pale Mh Rais Alipoingilia kati, baadaye walijiuzuru mawaziri Dr Mponda na Nw Lucy nkya

Ilitojea hivyo Kwa Wizara ya mambo ya ndani ,wizara ya utalii na wizara ya ulinzi,wizara ya elimu na wizara ya kilimo na mifugo katika saga la operashion tokomeza operation,operation kimbunga,matokeo mabovu ya wizara ya elimu,ubadhilifu na ufujaju wa wizara ya kilimo na ufugaji Mawaziri Dr Emanuel nchimbi,Shamsi Vuai nahodha,  Balozi Kagasheki,Ole medeyee n.k

Hii inaonyesha kukosekana kwa uungwana wa waziri mkuu katika dhana ya kuwajibika na uuwajibishwaji.

Uungwana ni vitendo natarajia katika hili la Ubadhirifu wa pesa za umma Ofisi ya waziri mkuu kupitia waziri mkuu mwenyewe itaongozwa na busara hekima na  vitendo vya kiungwana, kwa maslai mapana ya chama na serekali yetu tukufu.

0 comments:

Post a Comment