Facebook

Monday 24 November 2014

Njama ya polisi kumvua mwanamke Nguo yatibuka-Kenya

Afisa mmoja wa polisi wa utawala nchini
Kenya ni miongoni mwa wanaume
waliokamatwa kwa kujaribu kumvua nguo
mwanamke katika mtaa wa Komarock
viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Polisi walisema watu wanne walimsingira
mwanamke huyo alipokuwa anaenda nyumbani
kutoka kanisani akiwa ameandamana na rafiki
yake.

Wanaume hao walijaribu kumvua nguo mmoja
wa wanawake hao ila waliokolewa na wananchi
waliokuwa wakielekea makwao.
Wanaume wawili waliokuwa wanawaokoa
wanawake hao walijeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Daily
Nation, Kioo cha basi iliyokuwa barabarani pia
kilivunjika katika purukushanio hilo.
Polisi waliofika katika eneo la tukio waligundua
kuwa mmoja wa waliowashambulia wanawake
hao alikuwa afisa wa polisi.

Tukio hilo limefanyika siku chache tu baada ya
mamia ya wanawake kuandamana mjini Nairobi
kulaani kitendo cha kumvua mwanamke mmoja
mavazi yake yakisemekana kutokuwa na
heshima.

0 comments:

Post a Comment