Facebook

Friday 21 November 2014

Adebayor amtimua mamaake Nyumbani kwa tuhuma za uchawi.

Emmanuel Adebayor amuondoa mama yake kwenye nyumba kwa tuhuma za uchawi!!! Pamoja na kujulikana kote na kuchangia matatizo ya kijamii, nahodha wa timu ya taifa ya Togo,Sheyi Emmanuel Adebayor mzawa wa Lome hana mahusiano mazuri na famiia yake, na anasemekana kumtoa kwenye jumba lake lenye thamani ya dola za kimarekani 1.5 milioni mama yake Madam Alice Adebayor alilonunua kwa ajili ya familia.

Haya ni maneno ya binamu wake Adebayor Magaret alipokuwa akihojiwa na kituo cha Peace FM huko nchini Ghana.

“Kwa kipindi cha miaka sita sasa, Adebayor amemkataa mama yake na familia yake, akisaidia watu baki wasioihusu familia yake, na kumsema mama yake kuwa ni mchawi, Tumekuwa tukifikiria hali yake ya baadae kama mchezaji na hatukutaka kuweka jambo hili kwenye Vyombo vya habari, lakini sasa hii imepitiliza na hatuna jinsi, unaweza kuamini kuwa Ade alimtuma mlinzi wake wa nyumba kumtoa mama yake kwenye nyumba yake pamoja na familia yake huko Togo?

Hivi tunavyoongea mama yetu anaishi kwenye "apartment" aliyopangiwa na mdogo wetu wa mwisho anaeishi nchini Ujerumani Kola Adebayor.

Mama kila siku amekuwa ni mwenye kuishi kwa masikitiko na kulia kwa uchungu juu ya suala hili.kila siku mmoja wetu akimpigia simu na akagundua kuwa ni kati yetu, basi hukata simu haraka sana. “mimi binafsi nilisimamia ujenzi wa nyumba yake huko Trassaco na akatupa sehemu ya kukaa na mama kwenye nyumba hiyo, lakini cha kushangaza simu moja kamtuma mlinzi wake kuja kutufukuza kwenye nyumba.”

Mshambuliaji huyo mwenyewe alikiri kuwa hayupo vizuri na familia yake, na hakuna mawasiliano.

Akinukuliwa anasema. “Muulize dada yangu Margaret kama sikujenga nyumba yao huko East Legon, lakini nini kilitokea ?? nilimnunulia dada yangu mdogo Lucia gari la thamani ya dola 35,000,liko wapi?? kama wanataka yaishe waache kusambaza maneno na tukutane tuyamalize lakini wanaonekana hawataki kufanya hivyo, kwa nini wamekuwa wakisema kuwa sitoendelea mbele???..

Haya ni matatizo ya wachezaji wa Afrika, ama ni matatizo yetu waafrika? Shiriko nasi kwa kuacha comments zako chini.

0 comments:

Post a Comment