Facebook

Thursday 20 November 2014

"'WACATALUNYA WANAJIPENDA,WANAJIVUNA NA KUJIONA KAMA WAHAYA"

LIFAHAMU VIZURI JIMBO LA CATALUNYA INAKOTOKA BARCELONA LINAWEZA  KUJITENGA NA KUWA TAIFA HURU KUTOKA NCHI YA HISPANIA.

Location of Catalonia in Spain.
Kwa mtamshi au kwa lugha ya kimombo 'Pronaunciation' ya neno Catalunya huwa linatamkwa  hivi,wale mliokimbia 'Phonology' mtanisamehe /kætəˈloʊniə/

Kama ulikuwa hulijui jimbo hili la Catalunya,ngoja nikujuze kidogo kuhusiana na Jimbo hili.

Catalunya inakaliwa na watu wa jamii ya tofauti sana na jamii nyingine zilizo katika nchi ya Uhispania,Wacatalunya ni watu wanaojipenda sana,wanajivuna sana,wakiwa wamejaaliwa vipaji vya aina mbalimbali wangekuwa hapa kwetu nchini ningewafananisha na Watu wa kabila la kihaya.Kila kitu wanachofanya Wacatulunya wanaona ni bora zaidi kuliko wanachofanya watu wengine,wanafanana na wahaya katika mambo mengi sana.Wacatalunya wanajichukulia ni kama taifa  lililo ndani ya nchi ya Uhispania kutokana na nguvu kubwa iliyonayo.


 
Majimbo manne ya Catalunya Barcelona, Girona, Lleida na Tarragona

Catalunya imebeba jumla ya majimbo manne ambayo ni Barcelona, Girona, Lleida na Tarragona.Makao makuu ya Catalunya ni  Barcelona, ambalo pia ni Jiji kubwa kuliko hayo yote Manne.Vile vile Jiji hili la Barcelona ndilo Jiji kubwa la pili nchini Hispania ukiondoa Jiji la ma-raha Madrid.
 
Barcelona pia hivi sasa ndiyo kitovu cha shughuli mbalimbali barani Ulaya kama vile mahakama kubwa,shughuli za kiuchumi,kijamii,kiutalii likiwa limejiiamarisha vizuri katika nyanja zote za maisha.Hatimaye limekuwa miongoni mwa majiji muhimu na yanayovutia sana barani Ulaya.Tunarudi palepale ni kutokana na jinsi Wacatalunya wanavyojipenda hawapendi kuwekeza sehemu nyingine tofauti na Catalunya.Wamejenga na kuweka kila kitu katika Jimbo la Catalunya na kumvutia kila anayekwenda kulitembelea jimbo hilo.

Catalunya imejumuisha tawala mbalimbali zilizokuwa katika dola ya kale ya Catalunya ilyosambaratika katika vipindi tofauti tofauti

.Jimbo hili la Catalunya  limepakana na Nchi ya Ufaransa na Andora kwa Upande wa Kaskazini. Na eneo kubwa la Bahari ya  Mediterranean kwa upande wa Mashariki.

Lakini Pia liko jirani na Mkoa wa Aragana  upande wa kaskazini na Valencia upande wa magharibi.Lugha rasmi zinazotumiwa na wakazi wa jimbo wa Catalunya ni kicatalani ambacho ni tofauti sana na lugha kuu ya Uhispania na mara nyingi wachezaji wa klabu ya soka ya Barcelona wamekuwa wakiitumia lugha hiyo kitu ambacho kinaonekana kama ubaguzi kwa wachezaji ambao sio wazaliwa wa Catalunya.Lugha nyingine zinazotumiwa na Wacatalunya ni kihispaniola pamoja na kiaranese.


            Viongozi waliowahi kuitawala Catalunya

Catalunya ina historia kubwa sana kwani mnamo karne ya 10 baadhi ya majimbo ya Mashariki mwa Uhispania,yaani Gothia na Marca ya yalijipatia Uhuru wake kutoka chini ya Utawala wa Kifaransa yaani 'Frankish kingdom'.

Lakini ilipofika Mwaka 1137 Barcelona na  Aragon ambayo enzi hizo ilikuwa inafahamika kama 'The Crown of Aragon' yalikuwa ndani ya Jimbo la Catalunya ambalo lilikuwa bado halijaungana,lakini Barcelona sehemu ambapo kuna Wacatalunya wengi,waliona wivu kwa majimbo mengine kupata uhuru,kama walivyo Wacatalunya wanaojipenda na kujiona sana walijijenga kijamii,kiuchumi na kisiasa kwani baada ya kujipatia uhuru walitengeneza,walijijenga na kuwa eneo lenye nguvu zaidi katika safari za majini na ulinzi wa majini.

Na Wacatalunya walio Aragon nao walijijenga na kutengeneza mfumo bora wa kijeshi kupitia sera zao mbalimbali kama  "Main base for the Crown of Aragon's naval power and expansionism in the Mediterranean." Hiyo ni sera iliyosimamiwa vyema na kufanyiwa kazi na watu wa Aragon.

Katikati ya mwaka 1469 na 1516,aliyekuwa Mfalme wa Jimbo la  Aragon na aliyekuwa Malkia wa Castille (Madrid) waliamua Kuoana na kuyaunganisha majimbo yote yaliyo chini yao na kutengeneza utawala wa pamoja.Walifanikiwa kutengeneza na kusimamia  taasisi zote mbalimbali kama mahakama na katiba.

Kwa Bahati mbaya mnamo mwaka 1643-51 Vita vikali sana vilitokea.Vita hivyo vilijulikana kama  Reapers' War(1640–52),
Katika vita vile Catalunya wali hasi dhidi ya Uwepo wa majeshi ya Castille (Madrid) katika mipaka yao.Baadaya vita hivyo kudumu kwa takribani miaka 12 waliamua kukaa chini na kumaliza tofauti zao,na kisha wakasaini mkataba.

katika masharti ya Mkataba uliosainiwa kule  Pyreneesin(Valencia) 1659,ambao ulikua una amuru kumalizika kwa vita vilivyojulikana kama Franco-Spanish war.Castille walikubalianaga na Ufaransa kuachia mara moja jimbo lililo Magharibi mwa Catalunya.

Baada ya kumalizika na kupatikana na suluhu katika vita hiyo baada ya miaka 12 kulitokea vita nyingine iliyojulikana kama 'War of the Spanish Succession' (1701–14).Na katika vita hiyo Watu wa Aragon walikuwa wakipamba na Mfalme Philip V wa Uhispania, katika vita hiyo Wacatalunya wa Aragon walipigwa vibaya na Uhispania dola iliyokuwa imeanza kushika kasi baada ya kuunganishwa kwa baadhi ya Majimbo yanayozungumza kilatini kikiwa kimeunganishwa na kihispaniola.Hatimaye Wacatalunya wa Aragoni walishindwa na kikatalunywa kilipigwa marufuku na wakaamuriwa kuzungumza Kilatini kilichochanganyika na kihispaniola.

Ukiachana na na vita vya Napoleoni na vile vya Carlist,
Wacatalunya wamekuwa walipitia mabadiliko ya kiuchumi na mapinduzi ya viwanda mwaka 1913


Majimbo manne ya Catalunya yalitengeneza Jumuiya yao yenye dola inayojitegemea  iliyojengwa chini ya misingi ya kidemokrasia kipindi cha vita vya pili vya Uhispania "Spanish Republic War" (1931–39).

Kamanda wa Catalunya alirudi madarakani baada ya vita vya wenyewe yaani "Spanish Civil War" mwaka 1946 huku dola ya dikteta ya Kamanda Francios ilirudi madarakani na wakapiga Marufuku na kukomesha kabisa taasisi zote za KiCatalunya.

Na pia Kamanda François alipiga marufukua matumizi ya lugha ya KiCatalunya mnamo mwaka1950s and 1960s, Catalunya ilipiga sana hatua katika nyanja ya uchumi na kupata maendeleo makubwa  na hivyo ikawa sehemu muhimu sana kwa ajili ya shughuli za kitalii,huku ikivutia wafanyakazi mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za Uhispania na kuutengeneza mji mkubwa wa Catalunya uitwao Barcelona kuwa miongoni mwa kitovu kikubwa sana cha biashara barani Ulaya kikiwa kimejiimarisha pia katika sekta ya viwanda.

Tangia kipindi cha mpito Uhispania hadi kipindi cha demokrasia mwaka (1975–82).Catalunya imejijenga na kujiimarisha katika nyanja zote za maisha na hivi sasa ni kitovu kikubwa cha uchumi katika nchi ya Uhispania.
 
Mwaka jana Serikali ya Catalunya ilitangaza na kuweka wazi azma yao ya kutaka kujitenga na kuwa Taifa Huru.Ilikuwa taarifa mbaya zaidi kwa serikali ya Uhispania mwezi uliopita walipopiga kura za maoni ama Catalunya ijitenge na kuwa Taifa huru au iendelee kuwa Chini ya Nchi yaUhispania.

Mchakato wa kujitenga unaendelea lakini mpaka hivi sasa 
80% wanataka Catalunya liwe Taifa huru.Huku makao makuu ya Catalunya yatakua mjini Barcelona.

Kwa wale wapenzi wasoka watakuwa wanajua vizuri sana uhasama uliopo baina ya timu mbili kubwa zinazotawala soka la nchini Hispania kwa muda mrefu;Barcelona na Real Madrid

Ukiifuatilia makala hii nzuri utagundua yafuatayo:-
1-Uhasama baina ya Tim ya Real Madrid na  Barca ni wa kihistoria
2-Je Barcelona na Bilbao zitacheza tena La liga?
3-Je ni kweli tutarajie kuona taifa jipya lenye watu
wenye vipaji vya hali ya juu zaidi hasa katika Mpira wa miguu kuliko Hispania?


Binafsi siamini kama hili suala litatokea,kwani nina lilinganisha kama lile lililotokea Scotland walipokuwa wanataka kujitenga katika umoja wa dola ya Kiingereza (UNITED KINGDOM) ,lakini serikali ya inayoongozwa na David Cameroon ilipinga vikali suala hilo huku ilifikia hatua akenda Scotland kuwashawishi wananchi wasijitenge na kujitoa katika Umoja huo wa kihistoria.Lakini mwisho wa siku kura zilipigwa na Wascotland waliamua kubaki katika umoja wa dola ya Kiingereza.

Hakuna kikubwa viongozi tawala wanachoogopa kama kupoteza mapato na kushusha uchumi wa nchi zao Scotland ni muhimu sana katika kuongeza pato na uchumi wa Uingereza vivyo hivyo kwa Catalunya,ni mji mkubwa wapili kwa ukubwa Hispania ukiwa na vivutio mbalimbali vya utalii na mji mkubwa katika shughuli za kibiashara.
 
Ingawa suala la kujitengea kutoka katika nchi ya Hispania limekuwa suala linaloungwa mkono na wananchi na watu mashuhuri kutoka katika jimbo la Catalunya kama vile baadhi ya wachezaji wa Barcelona,wakiwemo kina Xavi Hernandez na Gerlard Pique na wengine wengi wamekuwa wakipigia sana chapuo suala hilo.

Haya yote yanatokea ni katika kutimiza kile kilichoanzishwa na mababu wa Catalunya,wakiendeleza mila na tamaduni zao za kujipenda,kujivuna na kujiona ni bora kuliko wengine.

Dunia inaenda kasi sana kila kukicha matukio mbalimbali yanatokea mwisho nasubiri kuona kama jambo hili litatimia lakini nabaki na maswali mengi kichwani kama jambo hili litatatokea kwani litakuwa linaleta faida ambazo ni chache na madhara makubwa kwa pande zote mbili katika nyanja mbalimbali za maisha.

     NAWASILISHA HOJA !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kusoma makala mbalimbali za kijamii,kiuchumi,kiasiasa,burudani na michezo.

Imeandaliwa na.......
                                 Katemi Methsela

0 comments:

Post a Comment