Facebook

Saturday 22 November 2014

Apson awatumia kina Bashe kumchafua Membe na Jack Gotham.

Nimeliona andiko la kumchafua Waziri
Membe na Jack Gotham lakini nataka
niwahakikishie tu kwamba halina chembe ya
ukweli hata kidogo.
1.

Ni kweli Jack Gotham yupo Dodoma na
tumekuja pamoja kwenye msiba wa baba yake
mdogo marehemu mzee Adolf, tumeingia
Dodoma Alhamis usiku saa 6 na tukapitiliza
msibani tukakaa mpaka saa 8 usiku ndipo
tuliporudi hotelini kujipumzisha.
Jana Ijumaa asubuhi na mapema tumedamka
kwenye maandalizi ya asubuhi pamoja na
matayarisho ya Ibada ambayo ilituchukua
muda mpaka saa 11 jioni ndipo tulipoelekea
makaburini kupumzisha mzee Adolf na kutoka
makaburi ya eneo la Kikuyu mnamo saa 1
kasoro.

Saa 2 tulikuwa Dodoma Carnival kwa ajili ya
chakula tukiwa watu zaidi ya 10 tuliotoka
msibani pasipokuwepo na mwanasiasa yoyote
katika jumuiko letu.Tumetoka huko saa 5
usiku na kurudi mahotelini.

Najiuliza ni muda gani matukio yote hayo
yaliyotajwa yametokea kwa aina hiyo ya
shughuli tangu juzi?Ni fabricated story yenye
lengo mahsusi ya kutaka kuharibu mahusiano
ya muda mrefu ya watu.

Ukweli uliopo ni kwamba yanayozungumzwa
ni siasa chafu za kundi la Lowassa
linaloongozwa na Apson Mwang'onda
aliyekuwa Dg wa Tiss miaka ya nyuma.Hii ni
baada ya kugundua kwamba sakata la Escrow
litawageukia maana limegusa baadhi ya watu
wao kama vile Andrew Chenge.

Pia jiulizeni je wanaoshabikia Escrow isomwe
bungeni ni wapambe wa nani?Kangi
Lugora,Deo Haule Filikunjombe na Peter
Serukamba wanajulikana wazi ni watu wa
Lowassa na sio Membe.Wanakosa hoja
wanabaki kutengeneza hekaya za kumchafua
Membe na Jack Gotham.

Apson Mwang'onda anapaswa aache
kuwatumia kina Bashe kufanya na kueneza
ujinga huu maana ataumbuka.

Asifikiri
anamharibia Membe au Jack zaidi
wanajiharibia wao na mtu wao.Asitake
tuongee ambayo yamebaki kuwa siri kwa nia
ya kuepuka mivurugano ndani ya chama na
serikali.

Akizidi kujilea katika umri wa ujinga wa
uzeeni tutamlipua kabla hata hawajafikiria
kumwambia mgombea wao aghairishe
kuchukua fomu.

Chanzo:Jamii Forum.

0 comments:

Post a Comment