Facebook

Monday 24 November 2014

WABUNGE WA CCM WAANDAA HOJA YA KUMNG'OA SPIKA MAKINDA.


Inaandaliwa hoja ya kumpigia spika kura ya kutokuwa na Imani nae, wabunge Wa ccm wanaanda mpango wametoka nje kumjadili kwa ubabe aliounesha asubuhi ya leo kwa kumzima Mh.Mbatia baada ya kutoa hoja ya kutaka hoja zote ziahirishwe na badala yake ijadiliwe hoja ya wizi wa ripoti ya PAC na alivyojipanga kuzima mjadala mzima wa scandal ya IPTL

Yule jamaa aliyekamatwa na ripoti ya escrow, bwana Mohamed Mbaruk atapaelekwa mahakamani ili kukidhi matakwa ya sheria ya kutojadili jambo linalo subiri uamuzi wa Mahakama,
wapinga ufisadi wameamua kuungana na wabunge Wa upinzani na huenda hoja hiyo ikawasilishwa leo jioni,pia mkakati wa kwenda jimboni kwake unaratibiwa vyema

SOURCE: Jamii Forum

0 comments:

Post a Comment