Kutoka kundi la Mapacha Watatu, Msanii wa Muziki Khaleed Chokoraa ameeleza kurejea na mabadiliko makubwa
katika muziki wao wa dansi.Mabadiliko hayo makubwa ikiwepo
kupunguza kutaja majina ya watu na vilevile urefu wa nyimbo
kinyume na vile ilivyokuwa imezoeleka katika nyimbo nyingi za dansi
hapa nchini.
Tuesday, 31 March 2015
Mapacha watatu waja na mabadiliko
Viongozi CECAFA wamuunga Mkono Blatter
Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), Leodegar Tenga amesema Rais wa Shirikisho la Soka
Ulimwenguni FIFA, Sepp Blatter amepewa nafasi na viongozi wa Soka
Barani Afrika katika kushinda Uchaguzi Mkuu wa FIFA.
Azam FC- Hatujamzuia Kavumbagu Kwenda Burundi
Uongozi wa Azam FC umesema haujamzuia mshambuliaji wake wa kimataifa, Didier Kavumbagu kurejea kwao kuitumikia timu yake ya taifa ‘Entamba Murugamba’.Katika taarifa yake, Msemaji wa Azam FC Jaffar Idd Maganga,amesema Kavumbagu yuko Tanzania kwa
sababu ya uzembe wa Shirikisho la Soka Burundi.
Maganga amesema, amesema shirikisho hilo liliwasiliana na uongozi wa Azam FC likimuomba Kavumbagu kwa ajili ya kuitumikia timu yake ya taifa katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA mwishoni mwa wiki hili tangu wakiwa Khartoum, Sudan wakicheza dhidi ya El-Merrikh,lakini mkali huyo wa mabao amekwama kwenda kutokana na kutotumiwa tiketi ya ndege.
Hili ndilo Tamko la Maaskofu kuhusu sakata la Gwajima
Maaskofu kutoka madhehebu mbali mbali ya Kikristo nchini Tanzania wanakusudia kuonana na mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu,
ili kupata suluhu kuhusu sakata linalomkabili mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, askofu Josephat Gwajima.
Aidha, maaskofu hao pia wameonyesha masikitiko ya kile walichodai
kuwa ni vituo vya polisi kutoonekana kuwa ni mahali salama kwa
watuhumiwa wa makosa mbali mbali wanaofikishwa hapo.
Askofu Gwajima amelazwa katima hospitali ya TMJ jijini Dar es
Salaam, alikopelekwa kwa matibabu baada ya kuanguka na kupoteza
fahamu wakati akihojiwa na polisi, kwa tuhuma za kumkashifu askofu
wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, Muadhama Kadinali
Polycarp Pengo.
Mchungaji Gwajima "Bastola iliyokamatwa ni yangu na nina imiliki kihalali.
Kuhusu wafuasi wake kukamatwa na bastola, Mchungaji Gwajima
amesema bastola hiyo ni mali yake halali anayoimiliki.
"Usiku wasiwasi ulizidi, huku kila mmoja akiwa hafahamu kwa nini ujumbe ule wa kuwa mimi nimefariki unasambazwa kwenye mitandao,
msambazaji ni nani, ana nia gani, ndio nikaamua kuwaagiza waniletee silaha yangu iliyokuwa kwenye begi ili likitokea lolote niweze kujilinda.
Ile bastola ni yangu na ninaimilki kihalali, hata nyaraka zake lakini ninawashangaa polisi hawajaja kuniuliza wala kuniomba document
zake”
Una lipi la kumwambia Gwajima .
BantuTz MAGAZETINI:SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO MACHI 31,2015.
BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.
Monday, 30 March 2015
Majambazi yavamia Kizuizi cha Polisi na sheli huko Kongowe-Mkuranga hivi punde.
Habari zilizotufikia BantuTz.com hivi punde kutoka eneo la Kongowe-Mkuranga mkoani Pwani.
Ni kwamba Majambazi wamevamia kizuizi cha polisi katika eneo la kongowe na kuuwa askari polisi wawili na kupora bunduki aina ya SMG mbili muda huu.
Pia baada ya tukio hili wamevamia sheli ya lake oil na kutokomea msitu wa vikindu mkuranga.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri.
Mchungaji Gwajima aondolewa chumba cha Wagonjwa mahututi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima
aondolewa katika chumba cha uangalizi Maalum (ICU) TMJ baada ya
kupata nafuu na hali yake kuendelea vizuri.
Dereva wa bodaboda anusurika kuuawa baada ya kupora mkoba.
kijana mmoja wa bodaboda maeneo ya Sinza
Afrikasana jijini DSM ambaye jina halikupatikana, alikoswakoswa
kuuawa baada ya kupora mkoba uliokuwa na simu ya mwanamke
aliyekuwa akipita njia.
Cha ajabu kijana huyo alivyokwapua mkoba,
pikipiki iligoma kuwaka basi raia wenye hasira kali wakaanza
kumshushia kipigo kikali.
Kijana aliponea chupuchupu kuchomwa moto,
kwani waliokuwa wamefuata mafuta ya petroli waliporudi walimkuta
trafiki akizuia asiuawe basi raia hao walihamishia hasira zao kwenye
kuichoma moto bodaboda ya kijana huyo.
CHICHARITO "REAL MADRID NI MAJANGA"
Mshambuliaji Javier Hernadez " "Chicharito" amesema kuendelea kukaa benchi katika klabu ya Real Madrid kunamfanya akose furaha na kukosa kujiamini.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya mwanzoni mwa msimu huu akitokea katika klabu ya Manchester United kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mzima.
Katika mkataba huo Real Madrid wanakipengele cha kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo lakini hana uhakika kama ataendelea kubaki klabuni hapo. "Ninajitahidi kwa asilimia 100 kwenye mazoezi lakini kwenye mechi sichezi,hilo linaondoa kujiamini na ninakosa furaha" alisema Chicharito
Tangu ajiunge na Real Madrid Chicharito amecheza mechi 13 za La Liga na kufanikiwa kufunga magoli matatu na kutoa pasi ya mwisho moja.
Chicharito,26, alijiunga na Real Madrid mara baada ya kukosa namba katika kikosi cha Louis Van Gaal na pia kuwasili kwa mshabuliaji Radamel Falcao kulichangia kwa kiasi kikubwa.
Mchezaji huyo ambaye mkataba wake katika klabu ya Manchester United unaisha June 2016 alifunga katika mechi ya kirafiki ya juzi jumamosi ambayo ilimalizika kwa Mexico kushinda 1-0 dhidi ya Ecuardo.
Wanyama na Mitrovic mbioni kujiunga Arsenal.
Kiungo wa kati wa Southampton Mugubi Wanyama
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati
wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa
Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini
Uingereza.
Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji
hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye
mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni
10.
Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na klabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa
amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea.
Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na
mchezo wake.
Sunday, 29 March 2015
TANZIA ABDU BONGE AFARIKI DUNIA.
Aliyewahi kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa kundi la Tip Top Connection, Abdu Bonge amefariki dunia ghafla usiku Wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.
Mmoja wa wasanii aliye kundi la Tip Top
Connection Madee, amesema kuwa bado hajafahamu chanzo cha kifo ila amefariki ghafla usiku huu akiwa nyumbani na msiba upo Manzese
Tip Top
RIP Abdu Bonge
Upagaji busu hadharani wapigwa marufuku India.
Kijiji kimoja nchini India kilichopo katika jimbo la kusini magharibi
kimepiga marufuku upigaji busu wa hadharani na tabia nyengine
mbaya.
Bunge la kijiji hicho kwa jina Salvador -de Mundo lililopo kilomita
maili nane kutoka kazkazini mwa mji mkuu wa Goa Panaji,lilipitisha
sheria hiyo kwa wingi likiwaonya watu wanaozuru eneo hilo dhidi ya
vitendo kama hivyo.
''Tumeidhinisha sheria hii kufuatia malalamishi kutoka kwa wakaazi
kuhusu wapenzi wanaopigana busu hadharani'',.Hii ndio hatua ya
kipekee ambayo itaweza kukabiliana na tatizo hilo'',naibu chifu wa
kiji hicho Reena Fernandes aliambia AFP.
Hatahivyo hakusema ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wakiukaji
wa sheria hiyo.
Hii ndiyo simu iliyotengenezwa kwa kutumia nyasi.
Watu wengi wamekuwa wakilalamikia teknolojia na ufundi wa simu
nyingi za kisasa wengi wakiwaponda wabunifu kwa misingi ya kuwa
asilimia kubwa ya simu za mfumo wa 3G na zaidi zinatengezwa kwa
plastiki.
Sasa basi,bwana mmoja mbunifu amekuja na jibu ya kutengeza simu
kutokana na ''Nyasi'' .
Bwana Sean Miles amezindua simu itakayokuwa ya kipekee.
Simu hiyo ndiyo ya kwanza kuwahi kutengenezwa kwa asilimia 100%
kutokana na bidhaa hai.
Gamba la juu la simu hiyo limeundwa kwa bidhaa inayotokana na
nyasi maalum iliyochanganywa na kemikali fulani na kiungo (resin)
"mchanganyiko huu maalum unatoa sura kama vile (carbon) alisema
Miles.
Mfumo huo unachanganywa na kumbwa kwa njia itakayoruhusu
watengezaji wa simu kuumba gamba la simu inayotokana na nyasi.
Simu nyingi za kisasa hazina ubunifu na zinaelekea kufanana
Bwana Miles alikuwa amepewa kandarasi na kampuni ya simu ya O2
kutafuta mbinu ya kutumia upya bidhaa ambazo zimekosa wateja
ama zimezeeka.
Hata hivyo kitengo cha ubunifu kilitamaushwa na ubunifu wake na
sasa kimeanza mikakati ya kutathmini uwezo wa kampuni hiyo kuunda
kwa wingi magamba ya simu.
Kufikia sasa asilimia 25% ya simu nzee nchini uingereza
zinarekebishwa na kutumiwa upya.
Huyu ndiye binadamu wa kwanza aliyepandikizwa Moyo wa binadamu aliyekufa.
Madaktari wa upasuaji huko Cambridgeshire wamefanya upandikizaji
wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa kutumia moyo mwengine
uliosimama kufanya kazi.
Myoyo hiyo hupatikana kutoka kwa watu waliokufa lakini ambao
myoyo yao bado inafanya kazi.
Katika upasuaji huo,moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye mapafu yake
na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.
Hospitali ya Papworth inasema kuwa mbinu hiyo huenda ikaongeza
idadi ya myoyo inayopatikana kwa asilimia 25.
Mgonjwa aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan, mwenye
umri wa miaka 60, kutoka London,alikabiliwa na shinikizo la moyo
mwaka 2008.
Alisema:kabla ya upasuaji,sikuweza kutembea na nilichoka sana,kwa
hakika siku na maisha mazuri.
Upandikizaji wa moyo
Lakini anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya yake
tangu upandikizaji huo.
Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku,na nimetembea hadi
haospitalini asubuhi hii bila tatizo.
Kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa myoyo katika kipindi cha
miaka 12 iliopita nchini Uingereza.
Lakini mahitaji yanashinda myoyo iliopo ,hivyobasi wagonjwa wengine
hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa.
Wengi ya wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana.
Saturday, 28 March 2015
Facebook kufungua huduma mpya kama "WhatsApp"
Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa wajenzi.
Habari hizo zilitangazwa na Mark
Zuckerberg katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco.
Zaidi ya programmu 40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga tayari zimeandaliwa kwa huduma hiyo.
Mtandao huo wa kijamii pia ulionyesha programu yake ya video inayomruhusu mtumiaji
kusukuma kamera huku kanda hiyo ikicheza.
SAKATA LA ESCROW LAMBURUZA KIGOGO WA RITA MAHAKAMANI.
Afisa Mtendaji MKuu wa Mamlaka ya Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA) Phillip Saliboko amefikishwa mahakamani kwa kupokea fedha
kiasi cha shilingi milioni 40, zilizochotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.
GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima
amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu
dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es
Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akiongea kabla ya kuhojiwa na polisi Mchungaji Gwajima amejitetea
kuwa alichofanya ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake
wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake katika makubaliano
waliofikia katika tamko la kuipigia kura ya hapana Katiba
inayopendekezwa.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani
Kardinali Pengo.
Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia
mitandao mbalimbali ya kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo
kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji
Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali
Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.
Thursday, 26 March 2015
Rais afanya uteuzi wa Wabunge wapya.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.
Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
Mhe. Janet Zebedayo Mbene
Mhe. Saada Salum Mkuya
Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
Mhe. James Fransis Mbatia
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
FRANCE v BRAZIL , STADE DE FRANCE LEO USIKU, KUKUMBUSHIA FAINALI YA 1998(WORLD CUP)
Siku ya Alhamisi Usiku katika dimba la Stade de France Jijini
Paris, ambako France Mwaka 1998
iliichapa Brazil 3-0 na kutwaa Kombe la
Dunia kwa mara ya kwanza na ya mwisho ,
ndio utakuwa Uwanja wa Mechi ya Kirafiki
kati ya miamba hao France na Brazil
ambao ni Mabingwa wa Dunia mara 5.
Ingawa Mechi hii ni ya Kirafiki lakini ni
muhimi kwa matayarisho ya Nchi hizi
kwani France ndio Wenyeji wa EURO 2016
Mwakani ambazo ndizo Fainali za Kombe
la Mataifa ya Nchi za Ulaya na Brazil
Mwezi Juni wako huko Chile kucheza Copa
America ambalo ndio Kombe la Mataifa ya
Nchi za Marekani ya Kusini .
Mara ya mwisho kwa Nchi hizi kukutana ni
Mwaka 2013 na Mabao ya Oscar , Hernanes
na Lucas Moura yaliwapa Brazil ushindi wa
3-0.
France , chini ya Kocha Didier Deschamps ,
watatinga kwenye Mechi hii bila ya
Wachezaji wao muhimu Kiungo Paul Pogba
na Kipa Hugo Lloris ambao ni Majeruhi
lakini wapo Mastaa wengine Kikosini kina
Patrice Evra, Antoine Griezmann na Karim
Benzèma.
Brazil, chini ya Kocha Dunga , wataongozwa
na Kapteni Neymar na Kikosini kwa mara
ya kwanza yupo Sentahafu wa Arsenal
Gabriel Paulista .
FAINALI YA COPA DEL RAY KUCHEZWA NOU CAMP, MADRID YAGOMA KUTOA UWANJA
Imeamuliwa kuwa Fainali ya Kombe la
Mfalme, Copa del Rey , itachezwa Nou
Camp, Nyumbani kwa Barcelona , hapo Mei
30 kati ya Athletic Bilbao na Barcelona.
Kawaida Fainali ya Kombe hili huchezwa
Uwanja usio wa Timu iliyo Fainali lakini
baada ya Real Madrid kugomea kutoa
Uwanja wao Santiago Bernabeu ukaanza
mvutano wa wapi Fainali hiyo ichezwe .
Kwenye Mkutano wa Shirikisho la Soka la
Spain na Klabu hizo mbili , Kura ilitumika na
Viwanja vya Sevilla , Vicente Calderon, na
Mestalla wa Valencia kubwagwa na kuacha
Viwanja vya Barca Nou Camp na San
Mames cha Bilbao kwenye kinyang ' anyiro .
Hatimae Nou Camp ilipita na hii itakuwa
mara ya kwanza kwa Timu iliyo Fainali
kucheza Fainali Uwanja wake wa
Nyumbani tangu 2002 wakati Deportivo La
Coruna walipoifunga Real Madrid Nyumbani
kwao Santiago Bernabeu .
Mara ya mwisho kwa Nou Camp kuwa
Mwenyeji wa Fainali za Copa del Rey ni
2010.
Ikiwa Barca watatwaa Kombe hili , ambalo
wao wanaongoza kwa kulibeba mara
nyingi , hii itakuwa mara yao ya 27 wakati
Athletic Bilbao wakifuata kwa wingi wa
kulitwaa kwa kulichukua mara 23.
Monday, 23 March 2015
NICASIUS COUTINHO SUSO:- MAMBO KUMI NILIYOJIFUNZA BAADA YA EL CLASSICO.
1. Kama kuna mtu mshale wake wa saa unaenda mbio kuliko wote duniani basi kabla ya Falcao ni Gareth Bale. Huyu kasharudisha chenji ya Perez katika misimu miwili hii, usitegemee kafara itamhusu mtu tofauti na yeye. Hata mimi binafsi sijaridhishwa na kiwango chake siku za karibuni achilia mbali ujinga wa Ronaldo dhidi yake. Hata yeye atakuwa anaitizama miwani ya Perez kwa umakini kuliko anavyomtizama mpenzi wake Emma Rhys Jones kwa husuda.
2. Ukishakuwa na Messi ndani unakuwa na wachezaji watatu kwa Sasa wa ziada ndani yake na yeye wa nne, unakuwa na winga, Kiungo mshambuliaji, Striker na jina lake mwenyewe ambalo ni hatari kuliko hivi vitatu vingine. Kumkaba huyu yataka moyo, vinginevyo ucheze mchezo mchafu tu wa madhambi. Madrid walivyofanya hivi kiasi walifanikiwa, Mancity hawakuwaza Hilo.
3. Luka Modric. Kipaji asilia. Huyu anakutana na tatizo kama la yule Bastian Schweinstiger. Dunia haina usawa kabisa, sio ajabu ukasikia Aaron Ramsey, Herrera, Henderson, Rakitic, na yule Oscar wanatajwa juu ya hawa. Acha Diamond aimbe Tatizo nyota wakati mwingine.
4. Huwezi kuwa/hapatokuwepo refa sahihi kuchezesha huu mchezo, presha haianzii uwanjani kwa mashabiki zaidi ya 80 elfu katika viwanja vyao wote, presha inakuja mpaka huku kwa mashabiki zaidi ya million tano wanaoutizama mchezo huu duniani, bahati mbaya hata wachezaji wanne ghali zaidi wapo huku. Napata shaka hata Perluig Collina kama angeweza kisawasawa.
5. Felipe Luis mbele ya Marcelo? Uongo anaoutumia Dunga ni kama ule wa Loew kumuaminisha Poldoski ni mchezaji anayetakiwa timu ya taifa Ujerumani kwa Sasa. Tatizo kubwa la Marcelo lilikuwa ukabaji lakini kwa Sasa amekuwa moja ya mabeki bora wa ulinzi Pembeni, achilia mbali kuwa ndo beki bora zaidi linapokuja suala la ushambuliaji. Hata hivyo Ile staili yake ya siku ulinifurahisha zaidi, ilikuwa tamu kuliko goli la Suarez.
6. Kuna Neymar wawili duniani. Mmoja yupo timu ya taifa, mwingine Barcelona. Siku huyu wa Barcelona akimuiga tule wa timu ya taifa Brazil, basi Ana miaka miwili kuchukua Ballon D Or, akiwaacha Hawa wamalizie muda wao. Wakati huo namba tatu itakuwa yake.
7. Ningekuwa na mawasiliano na Anceloti ningemwambia tu, ni bora Israel wawaamini wapalestina kuliko yeye kumuamini Perez. Aachane na Mourinho akamuulize Capello baada ya kuchukua ubingwa nini kilifuata. Ni rahisi kufanya majadiliano na Abramovich kuliko huyu.
8. Isco... Del Bosque Kuna kichwa tu. Kuna watoto wanakera sana, wakati unamuwaza Silva, Navas, Mata yeye anakupa sababu ya ulimwengu kukunyooshea kidole, kumuacha huyu kikosi cha kwanza achilia mbali timu ya taifa unatakiwa uwe na roho ya Hitler. Hata Anceloti najua anaumwa kichwa akirudi James itakuwaje.
9. Kareem Benzema, umefika muda sasa, umeshinda kila kitu katika klabu, waachie ufalme wao. Pishana na yule Falcao uende ukajichukulie ufalme pale Manchester au sogea pale Liverpool, si unamuona Sanchez. Hata akiwa katika kiwango kibovu mashabiki wanainama na kumsujudia. Alichokifuata Suarez Barcelona ndicho ulichonazo, na akichokipata Anfield ndicho unachokikosa. Kuitwa mfalme katika nchi inayokuhusudu.
10. De Gea endelea kugomea mkataba mpya United. Sio muda utatakiwa ukachukue Ile nafasi madrid, haina maana kuwa Casillas alicheza vibaya Ila unaona hata uhamasishaji wake golini umeshuka sana.
NB:
Usiniulize kwanini hayapo ya Manchester United vs Liverpool. Yule Mata kajibu makala yangu ya wiki iliyopita, Fellaini kajibu uchambuzi wangu wa sports bar na sports xtra. Hata hivyo yule Blind Hana adabu achilia mbali ubora wake ambao wengi hawausemi, Ile chenga alompiga Emre Can inahitaji uwe umesoma vizuri hesabu kuifanya na kuizuia. Wanaweza wanaotumia mikono tu (basketball). Huu sio wakati mzuri kukutana na Man United, wanakaba vizuri kuanzia kwenye nusu yao, na wanatengeneza mgawanyo mzuri wa mashambulizi. Sema kinachokera Mata anaweza kurudi benchi au Herrera. Hapo tu.
Yule Gerrard napata shaka hata mechi ya kumuaga atakuwa na tukio yule.
Siku Raheem akitaka tena 140 mwambieni haipatikani vile. Yule Coutinho mkataba waliompa unamlinda kuja kuondoka kwa kitita kikubwa.
Ahsanteni. By Nicasius Coutinho Suso
Sunday, 22 March 2015
CLASH OF THE TITANS: UCHAMBUZI WA MECHI YA EL CLASSICO NA Mr.CHOI (KAA TAARIFA YAKO)
EL-CLASSICO ² 23:00
BLAUGRANA vs BLANCOS
Wakiwa katika dimba la Camp Nou lenye kuchukuwa watazamaji 99,354 huku wakishinda michezo 89 na kutoa sare 48 wakipoteza mara 92 Barcelona watawakabili Real na kujaribu kutafuta ushindi wa 90 ktk El Classico.
Blaugrana wana pointi 65 huku Blancos wakishika nafasi ya pili kwa pointi 64 katika michezo mitano ya hivi karibuni kwenye mashindano mbalimbali Blancos wamekuwa wababe mbele ya Blaugrana kwani wameshinda mara tatu kati ya mbili walizo shinda Blaugrana na mchezo wa awamu ya kwanza Blancos walishinda 3-1.
Ni miongoni mwa mchezo wenye kuteka hisia kubwa za mashabiki wa soka ulimwenguni kote si upinzani wa timu hizi tu bali hata upinzani wa safu za ushambuliaji kwa pande zote MSN-INTERNATIONAL ya Blaugrana na BBC ya Blancos pia sio safu hizo tu bali upinzani mwingine wa MESSI na C.Ronaldo.
Messi ni kinara wa magoli La-Liga akiwa na magoli 32 dhidi ya 31 ya mpinzani wake Ronaldo hivyo licha ya upinzani wa timu hizi katka pointi tutaraji kuona wachezaji hawa kila mmoja akionesha umwamba mbele ya mwenzake.
Cr7 ameshafunga magoli 6 ktk michezo 7 ndani ya Camp Nou huku akifunga mara 8 katika michuano yote na historia inaonesha amesha funga magoli 14 tangu atue Real na kucheza El Classico, tangu achukue tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mwaka jana kiwango chake kimeonekana kushuka hasa kwa upande wa kuzifumania nyavu tofauti na mpinzani na hii leo endapo atafunga atafikisha goli la 15 sawa na Raul kwenye El Classico.
Real wakiwa hawana matokeo mazuri kwa siku za hivi karibuni ndo timu pekee ilio ifunga Barca magoli mengi msimu huu (3-1) lakini pia watashuka dimbani kuitafuta historia ya mwaka 1978 kuifunga Barca mara tatu mfululizo kwenye El Classico kwani mwezi 10/2014 waliwafunga 3-1 na mwezi wa 4/2014 waliwafunga 2-1 ktk kombe la mfalme.
Mara nyingi Real ama Blancos wamekuwa na asilimia 38 ya matokeo mazuri mbele ya Barca kipindi cha kwanza cha mchezo huku wapinzani wao asilimia 53 ya kipindi cha pili na zilizo baki ni sare. Majeruhi ni James lakini asilimia kubwa ya kikosi kipo fiti na tunataraji kuona Modriç na Kross wakicheza kati huku vita vikubwa vikiwa kwa Pepe na Suarez, Marcelo na Messi ingawa hofu ya Real ni golikipa Cassilas kwani amekuwa akifanya makosa sana golini.
Blaugrana ama Barcelona wana Catalan wanaingia ktk mchezo huu wakiwa katika kiwango bora kwa sasa kikichagizwa na Messi alie funga magoli 17 kwenye michezo 11 La-liga tangu mwaka uanze,hawana majeraha ktk kikosi chao hasa kilicho cheza siku za hivi karibuni huku Busquets akirejea ingawa anaweza asipangwe leo na nafasi yake kucheza Mascherano.
Mara nyingi Barca wakikutana na Real hasa siku za hivi karibuni safu yao ya ulinzi ndo imekuwa tatizo kwa kushindwa kuendana na kasi ya Cr7 na Bale ambao kwa staili ya mashambulizi ya kushtukiza na ya kasi wamekuwa na madhara sana.
Pique ambae mara nyingi amekuwa akisababisha madhara kwa kushindwa kasi ya mchezo kwa hivi sasa yupo katika kiwango kizuri na uzuri huo atahitajika kudhirisha mbele ya BBC huku akitaraji simama na Mathieu.
Wameruhusu magoli 16 mpaka sasa huku wakifunga magoli 78 pengine rekodi hiyo nzuri itawawezesha kuiboresha zaidi mbele ya Real.
Magoli mengi ya Barca wamefunga hasa ndani ya kumi na nane tofauti na Madrid ambao wanaonekana kufunga hasa nje ya kumi na nane. Mara ya mwisho Barca kupoteza michezo mingi ktk dimba la nyumbani ni msimu wa 2007/8 kipindi yupo Rijkaard baada ya kupoteza mara 3 kwenye ligi.
Kiujumla mchezo utakuwa wa kasi sana kutokana na ushindani kwenye msimamo wa ligi Ratic, Iniesta katika safu ya kiungo cha juu na Modriç,Isco wote hawa wanatarajiwa kuonesha ufundi wa hali ya juu achilia mbali safu zao za MSN na BBC ambapo mpaka sasa MSN wanagoli 56 katika ligi na BBC wanagoli 55 zote ktk ligi pekee.
For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com