Facebook

Thursday 4 June 2015

Chris Brown akanusha taarifa za kuvuta bangi ndani ya ndege.


ChrisBrownPlaneMain-559x520
Baada ya Mmoja wa wafanyakazi wa ndege aliyo kodi Chris alisikikika akisema, “Nilimsikia Chris akisema nimelipia hii ndege dola 60,000 Kwa hiyo ninaimiliki kila kitu na hawa watu humu ndani ni wangu, huku akitoa moshi wa bangi aliyokua akiivuta”.
Kufuatia kusambaa kwa habari kuendelea kwamba Mkali wa R&B nchini marekani, Chriss Brown amevuta bangi ndani ya ndege na kupulizia moshi wa bangi kioo cha ndege , Jet aliyoikodisha kwa ajili ya safari ya utalii na kundi la vijana wenzake, ameibuka na kukanusha kwamba hakuwahi kufanya kitendo hicho.
Chris amechukizwa na habari hizo zinazotokea na kusambazwa kila kukicha kitendo ambacho amedai kinamfanya ajichukie hata yeye mwenyewe.
“Kuna muda mwingine naenda kwenye kioo kujiangalia, na najikuta naichukia taswira ninayoiona kwenye kioo”, alisema Chris Brown.
Mmoja wa vijana walio kuwepo pamaja na Chris alisema, “Hakuna kitu kama hicho, hizo ni stori za uzushi kabisa. Chriss alivuta sigara nje ya ndege kabla ya safari na hakuvuta bangi akiwa ndani ya ndege”

0 comments:

Post a Comment