Facebook

Saturday 6 June 2015

TFFyaingilia kati mgogoro wa Simba SC na Singano 'Messi'


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’(pichani)na klabu yake,Simba SC.
Taarifa ya TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne Juin 9, mwaka huu kwa mazungumzo.
“Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo, TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania,”imesema taarifa ya TFF.
Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo kwamba imeghushi Mkataba wake.
Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika mwakani.
Na Messi si mchezaji wa kwanza kuishutumu Simba SC kughushi Mkataba wake, kwani wachezaji wengine za zamani wa klabu hiyo Athumani Iddi ‘Chuji’ naKevin Yondan wamewahi kutoa malalamiko kama hayo wakati wanahamia kwa mahasimu, Yanga SC.

0 comments:

Post a Comment