Facebook

Thursday, 4 June 2015

Pogba-"Ndoto zangu ni kucheza na Messi"


KIUNGO wa Juventus, Paul Pogba amekiri kuwa ana ndoto za kucheza sambamba na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka jijini Turin huku Barcelona na Real Madrid zikitajwa kuwa na nia ya kumsajili.
Pogba sasa ameweka wazi jinsi anavyoihusudu Barcelona ambao watakuwa wapinzani wao katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi hii.Nyota huyo alikaririwa akidai kuwa kucheza pamoja na Messi itakuwa ni kutimiza ndoto zake kuwa kweli kwasababu ni mchezaji bora duniani.
Pogba aliendelea kudai kuwa anajua Barcelona wanapewa nafasi kubwa kuwa mabingwa katika mchezo wao ujao lakini watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo

0 comments:

Post a Comment