Facebook

Thursday, 4 June 2015

Marekani yakiri kusambaza vidudu hatari vya kimeta.

Maofisa wa ulinzi nchini marekani wamekiri kuwa maabara kadhaa zilizopokea kimakosa sampuli hai za vidudu hatari vya kimeta ni zaidi ya mara mbili ya matarajio ya awali.
Pentagon imesema vifaa hamsini na moja katika majimbo kumi na saba nchini Marekani, pamoja na maabara zilizopo nchini Canada, Australia na Korea kusini walitumiwa sampuli hizo kutoka maabara ya jeshi la marekani.
Imesema usafirishaji wa vijidudu hivyo vilianza miongo kadhaa iliiyopita na iliendelea mpaka wiki iliyopita.
Hadi sasa hakuna mtu aliyeathirika lakini zaidi ya watu ishirini walikuwa wakibeba sampuli hizo wamekuwa wakitibiwa kwa tahadhari tu.

Related Posts:

  • Kiongozi wa upinzani Ethiopia aonyeshwa kwenye TV Andargachew Tsege alikamatwa akiwa safariki kutoka Milki za kiarabu Kiongozi wa upinzani nchini Ethiopia, Andargachew Tsege, ameonekana kwenye televishen… Read More
  • Makanisa kupunguzwa Burundi     Bunge la Burundi limepitisha muswada unaolenga kupambana na "mfumuko wa makanisa" nchini humo. Utafiti wa serikali mwaka jana uligundua kuwepo na madhehebu 557. Sheria mpya zinataka makanisa kuwa na wafua… Read More
  • Viongozi wa Usalama Somalia wafukuzwa kazi. Maafisa wakuu wa usalama na wa polisi wamefukuzwa kazi kufuatia kundi la al-Shabab kushambulia ikulu ya Somalia, amesema waziri mmoja. Washambuliaji watatu waliuawa na wa nne kukamatwa, imesema ofisi ya rais. Al-Shaba… Read More
  • AL Shabaab washambulia ikulu Somalia wapiganaji wa AL shabaab Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu kuishambulia. Maafisa wanasema washambuliaji wapa… Read More
  • 20 wauawa katika shambulio la anga, Gaza Mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel yamewaua zaidi ya watu 20 katika eneo la Gaza, wakiwemo raia. mashambulio hayo yanatazamiwa kuwa mwanzo tu wa oparesheni kubwa inayopangwa kufanywa na Is… Read More

0 comments:

Post a Comment