Facebook

Tuesday 2 June 2015

UCHAMBUZI:Fainali Ligi ya mabingwa barani Ulaya Barcelona vs Juventus Na Mr.Choi

Muda unazidi kusogea pasipo kuchelewa tulianzishe mkongwe beki tatu niliyo ikubali sana enzi zako

MALDIN-Barcelona ama ukipenda waite Blaugrana ilianzishwa miaka 115 iliyopita 29/11/1899 na kama ulikuwa hufamu wanzilishi wa timu hii ni raia wa Uswisi wakiongozwa na Joan Gamper (Hans-Max Gamper) huyu alikuwa mwanasoka pia mcheza Rugby alisha kipiga Fc Basel akiwa kama keptaini,Fc Zurich kisha alipo timkia Jiji la Barcelona 22/10/1898 kumsalimia mjomba wake Emili Gaissert akiwa anajishuhulisha na shughuli mbalimbali na ndipo wazo likaja kisha akafanikisha lengo lake na ukawa mwanzo wa Barcelona na chini ya uongozi wake walichukua kombe la mfalme mara 3 (1911-12,1912-113,1924-25)

  CHOI- Du hiyo balaa ingawa najua yapo mengi inabidi tuangazie utamu wa juu,Juventus wao hupenda sana kuitwa "Vecchia Signora" kibibi kizee timu hii ilianzishwa miaka 117 iliyopita 1/11/1897 yani kipindi ina anzishwa ndo kwanza Mzee Gamper alikuwa hajapata wazo la Barcelona sasa hawa walianzishwa na kundi la wanafunzi wakiongozwa Eugenio Canfari na kaka yake Enrico yani dizaini msoto wa kitaa wanacheza-cheza tu ila mwisho wa siku hao majamaa wakawa na fikra za kuwa na timu na mwisho wa siku fikra zao ndo tunaiona Juventus hadi leo.

MALDIN-Misoto ipo mingi na mafanikio yalizidi kuonekana sasa tukirejea upande wa kombe la Mabingwa Barcelona ubingwa wao wa kwanza walichukua katika muda wa nyongeza dhidi ya Sampdoria fainali zilizo fanyika  Wembley goli hilo pekee lilifungwa na kocha wa hivi wa Southampton Ronald Koeman kwa mkwaju wa faulo hiyo ilikuwa 20/05/1992.

   CHOI- Noma sana ngoja tulisongeshe kumbuka Kibibi hiki ubingwa wao wa kwanza ilikuwa 29/5/1985 kule Brussels dimba la Heysel nao pia waliibuka na ushindi finyu goli moja ambalo lilifungwa na Raisi wa sasa wa Uefa mpinzani wa Blatter Michel Platin kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 hawa walionja radha mapema kuliko wana wa Catalunya.

  MALDIN-Haya sasa ubingwa wa pili wamechukua miaka hii ambayo mpira umesambaa sana ilikuwa tarehe 17/5/2006  kama unakumbuka fainal wali kitwanga na Arsenal iliyo kuwa bora sana Campbell alianza kuifungia Arsenal dakika ya 37 ila Etoo enzi hizo akiwa wa moto akatupia dakika ya 76 kufumba macho kufumbua Belletti mnamo dakika ya 81 akafunga mahesabu pale Stade de France Paris nyumbani kwa Mzee Wenger  wakati huo Henry akifanya yake huku Bibi yangu akisuuzika na Ronaldinho.

   CHOI- Sasa mkongwe wajua wakati Barcelona wakiwa wametwaa mara ya kwanza wenzao Juventus katika dimba la nyumbani Italy pale Roma Stadio Olumpico hiyo ni 22/5/1996 walitwaa ubingwa wa pili kwa njia ya mikwaju ya penalti dhidi ya Ajax , hapo Ajax ilikuwa na wakali kama Jari Litmanen alie ibuka mfungaji bora wa michuano (9) kina Patrick Kluivert upande wa Juventus walikuwa kina Ravanelli na mfalme Alessandro Del Piero.
      Na hapo ndipo ukawa ukurasa wao umefungwa wa kutwaa ubingwa huu.

   MALDIN-Haya wewe pumzika, sasa msimu wa 2008-09 wana wa Catalunya waliendelea fanya yao na safari hii ilikuwa pale Olimpico Jijini Roma  tarehe 27/5/2009 kwa kuicharaza Manchester United 2-0 magoli ya Etoo dakika ya 10 na Messi  dakika ya 70  msimu ambao Messi alikuwa mfungaji bora kwa kuwa na magoli 9 katika dakika 982 alizocheza fainal.

   MALDIN- Choi naona umetulia tu ngoja nimalizie safari hii wakarejea tena Wembley uso kwa uso na Manchester ambayo ilikuwa na shahuku ya kulipiza kisasi kile cha msimu wa 2009 sasa badala ya kulipiza kisasi kibao kikageuka kwa vijana wa Ferguson kukunyugwa goli 3-1  hiyo ni tarehe 28/05/2011 goli za Pedro 27 kisha Rooney akasawazisha dakika ya 34 kumbe wakawa wamechokoza moto,Messi  akatupia dakika ya 54 na David Villa 69.
      Msimu huo Messi alikuwa mfungaji bora kwa goli 12 ndani ya dakika 1098 alizo cheza kwenye michuano hiyo .

   CHOI-Nakumbuka fainal hiyo nilikuwa na Bibi yangu sasa alipo muona Ferguson anatetemeka mikono akanijuza kumbe hata Ulaya huwa wanauwa mijusi maana wazee wetu huamini ukiuwa mijusi basi uzeeni utatetemeka mikono nikamjuza Xavi anakinukisha mzee anaona
Maluelue anapagawa kwa pasi za wana wa Guardiola

   MALDIN-Mimi sipo huko ila tambua tangu msimu mpya wa 1992  Barcelona wamechukua mara nyingi zaidi ubingwa huu mara nne zaidi ya vilabu vingine.

KWA MAONI::
    Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment