Facebook

Friday 5 June 2015

Tetesi zote za Usajili barani Ulaya siku ya leo.

Winga wa England Raheem Sterling, 20 hana tatizo na uwezekano wa kuhamia Manchester United kutoka Liverpool, ingawa mchezaji huyo
ana wasiwasi kuhusu jinsi uhamisho huo utakavyopokelewa, kwa kuzingatia uhasama baina ya timu hizo mbili (Guardian),

Liverpool wanasisitiza kuwa hawatofanya biashara yoyote na mahasimu wao wa Manchester (Liverpool Echo),

Radamel Falcao, 29, anataka kukamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea kabla ya michuano ya Copa America kuanza Juni 14 (Daily Telegraph),

Dick Advocaat atapewa pauni milioni 50 za kukijenga kikosi cha Sunderland baada ya kukubali kuongeza mkataba wake wa kuwafunza Paka Weusi (daily Mirror),

Beki wa Bayern Munich kutoka Brazil, Dante, 31 amekataa kuhamia Manchester United baada ya kusema ana nafasi ya kushinda makombe mengi zaidi akiwa na klabu yake ya Ujerumani (Daily Star),

Manchester United wapo tayari kumuuza Nani msimu huu na huenda akaelekea Inter Milan na sio Sporting ambapo amecheza kwa mkopo msimu uliopita (Independent),

Sampdoria ya Seria A inajiandaa kumsajili beki wa kati wa Chelsea Kurt Zouma, 20 kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo ya Italia (Metro),

Dani Alves, 32, amekubali mkataba wa awali na Manchester United na atahamia Uingereza tarehe 1 Julai (Daily Star),

kiungo wa Southampton, Victor Wanyama, 23 amesema "itakuwa vizuri" kujiunga na Arsenal (Daily Mail),

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers imeripotiwa amemfukuza mwalimu wa kikosi cha kwanza Mike Marsh (Sun),

Mshambuliaji wa QPR Charlie Austin anasakwa na Tottenham, Newcastle, Aston Villa na Southampton kwa pauni milioni 10 na ameonesha ishara kuwa yuko tayari kuihama klabu yake iliyoshuka daraja (Daily Express),

Arsenal wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 25 kumsajili kiungo wa Monaco Geoffrey Kongodbia, 22, ikiwa watamkosa Morgan Shneiderlin wa Southampton (Independent),

Liverpool wamepata matumaini makubwa
ya kumsajili kipa wa Sporting Lisbon, Rui Patricio, 23 baada ya klabu hiyo ya Ureno kumsajili Azbe Jug kutoka Slovenia (Daily Express),

Manchester United wanajiandaa kumsajili kipa wa Galatasaray Fernando Mulsera, 28, kuziba nafasi ya David De Gea anayeelekea Real Madrid (Metro),

Wakati huohuo winga wa Manchester United
Ashely Young, 29 anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu mwezi ujao kusalia Old Trafford (Daily Mirror),

Paris St-Germain wamemfanya winga wa Manchester United Angel Di Maria, 27, kuwa
mchezaji kipaumbele wa kumsajili msimu ujao (TalkSport),

Hata hivyo Di Maria amesema atasalia Old Trafford msimu ujao licha ya kutokuwa na msimu mzuri (Sun),

Beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 28,
anapanga kusaini mkataba mpya msimu ujao Tottenham, licha ya kuhusishwa na kuhamia Napoli (Times).

Habari zilizothibitishwa za uhamisho tutakufahamisha zitakapothibitishwa.

0 comments:

Post a Comment