Facebook

Wednesday 3 June 2015

Kujibadili jinsia kwa Baba wa kambo wa Kim Kardashian hakujaishia hapo,hivi sasa abadili muonekano na jina lake.

caity
Moja ya familia zisizoishiwa vituko na kila mara kuingia kwenye headlines ni pamoja na familia ya Kriss Jenner ambaye ni mama mzazi wa staa maarufu duniani Kim Kardashian.
Baada ya kusambaa kwa muda mrefu habari kuhusu kujibadilisha jinsia kwa baba wa kambo wa Kim Kardashian, aitwaye Bruce Jenner, sasa ni rasmi kuwa baba huyo amejibadilisha jinsia yake na sasa anajulikana kama Caitlyn Jenner.
bruc2
Uamuzi huo umevuta hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia umeonekana kupokelewa  tofauti na familia ya akina Kardashian.. mkewe wa zamani ambaye ni Kriss Jenner na familia yake wameonekana kutopendezwa na uamuzi huo japo yeye mwenyewe hana tatizo kabisa na ishu hiyo kama ambavyo wengine wanamchukulia.
bruc
Katika Ukurasa wake mpya wa Twitter alioufungua muda mfupi baada ya kujitangaza na kupata followers wengi, Bruce Jenner ameonesha kufurahishwa na hatua aliyofikia hivi sasa.
kkk

0 comments:

Post a Comment