Facebook

Wednesday 3 June 2015

Berbatov afungashiwa virago Monaco.


MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa waBulgaria, Dimitar Berbatov anatafuta timu ya tatu ya kujiunganayo England, baada yakutemwa na AS Monacoya Ufaransa.

Berbatov alijiunga na vigogo hao wa Ligue 1 Januari mwaka 2014 kutoka Fulham ya England na atakumbukwa kwa kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-1 kwenye dhidi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa yuko huru baada ya kuachwa na Monaco, iliyomaliza katkka nafasi ya tatu kwenye Ligue 1 msimu huu.

Katika taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim Vasilyev, amesema;"Dimitar Berbatov ameonyesha kipaji chake chote na soka babu kubwa.

Dhahiri ni miongoni mwa washambuliaji wakubwa waliojiunga na AS Monaco. Tunajivunia alicholeta katika klabu na tunamtakia kila la heri aendako,".'

0 comments:

Post a Comment