Facebook

Wednesday 3 June 2015

Liverpool yamkosa mshambuliaji hatari Lacazette

Timu ya Liverpool itashindwa kumsaini mchezji Alexandre Lacazette ,baada ya Rais wa timu ya Lyon Jean-Michel Aulas kusema mchezaji wake hatojiunga na Liverpool kufuatia timu hiyo ya Anfield kukosa nafasi ya kushiriki Champions League msimu ujao.
Mchezaji huyo amefunga magoli 27 katika Ligue 1 msimu huu pia anafuatiliwa na miamba mingine ya Premier League timu za Arsenal, Newcastle na Tottenham.
kwa upande wake Brendan Rodgers amesikitishwa na maamuzi hayo baada ya kushindwa kuipa timu yake nafasi ya kushiriki klabu bingwa Ulaya.
 

Je ! unadhani mchezaji Lacazette ni chaguo bora kwa Liverpool kwa msimu ujao wa EPL katika kurudisha heshima Anfield.

0 comments:

Post a Comment