Facebook

Wednesday 3 June 2015

Jack Wilshare ashtakiwa na FA.


Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ameshtakiwa na chama cha soka cha England, FA kufuatia tukio la kwenye msafara wa basi wakati wa kusherekea ushindi wa Kombe la FA.
Taarifa ya FA imesema: "Inatuhumiwa kuwa tabia yake ya kufanya na/au kutoa maneno ya uchochezi katika ziara ya ushindi haikuwa muafaka na/ au kutia doa mchezo wa soka."
Wilshere ana hadi Juni 10 saa 12 jioni saa za Uingereza kujibu shtaka hilo.
Arsenal iliamua kutomchukulia hatua yoyote Wilshere, lakini ilimkumbusha kuhusu majukumu yake.

0 comments:

Post a Comment