Facebook

Thursday 4 June 2015

Hizi ni tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo.

Manchester United wanakaribia kutoa dau la pauni milioni 25 kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, 20 (Mirror),

Chelsea wanataka kumsajili Radamel Falcao kwa mkopo kutoka Monaco. Falcao, 29, amefunga mabao manne katika mechi 29 akiichezea Manchester United kwa mkopo msimu uliopita (Daily Star),

kiungo wa Juventus, Andrea Pirlo, 36 anajiandaa kujiunga na klabu ya New York City FC ya ligi ya Marekani ya MLS ambayo Frank Lampard pia ataichezea. Pirlo alikuwa amehusishwa na kuhamia Liverpool au Chelsea (AS),

kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba, 22 atajiunga na Barcelona msimu ujao. Manchester City walikuwa tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili mchezaji huyo wa Juventus ambaye anatarajiwa kucheza fainali ya klabu Bingwa Ulaya siku ya Jumamosi dhidi ya Bacra (Daily Star),

Dimitar Berbatov, 34 anataka kurejea England baada ya mkataba wake kumalizika Monaco (Sky Sports),

Arsenal wapo tayari kupambana na Inter Milan kumwania kiungo mkabaji wa Monaco Geoffrey Kongodbia, 22 (Mirror),

Hata hivyo kiungo wa Southampton Victor Wanyama wamesema "itakuwa vizuri" akijiunga na washindi hao wa Kombe la FA (DailyStar),

Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 22, amesema ana furahia kusalia katika klabu hiyo licha ya kusisitiza kuwa angependa kucheza Champions League (Liverpool Echo),

kiungo wa zamani wa Newcastle Yohan Cabaye, 29, amekataa uwezekano wa kuhamia Aston Villa lakini anataka kwenda Crystal Palace kuungana na meneja wake wa zamani Alan Pardew (The Sun),

Manchester United wanamtaka kipa wa Tottenham Hotspur Hugo Lloris, 28 kuziba nafasi ya David De Gea, 24 iwapo atajiunga na Real Madrid (Manchester Evening News), lakini Real Madrid bado hawajatangaza dau rasmi kwa De Gea (Express),

kipa wa Chelsea Petr Cech, 33, atafanya uamuzi wa hatma yake baada ya mechi ya timu yake ya taifa dhidi ya Iceland Juni12 (The Sun)

kiungo wa Bosnia Herzegovina Miralem Pjanic amemtaka mchezaji mwenzake wa timu ya taifa Edin Dzeko kumfuata Roma msimu ujao (Daily Mail),

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 20, amesema kikosi cha Liverpool ni kizuri cha kuweza kushinda Ligi Kuuya England (Sky Sports),

Meneja wa West Brom, Tony Pulis amesema kuitwa kwa Saido Berahino katika kikosi cha England cha chini ya miaka 21 ni hatua nzuri kwa maendeleo ya mchezaji huyo mzaliwa wa Burundi (Birmingham Mail).

0 comments:

Post a Comment