Facebook

Monday, 1 June 2015

Ujumbe wa Rio Ferdinand baada ya kutundika jaruba.

yeye
Akiwa bado kwenye majonzi makubwa ya mkewe aliyefariki duniani mwanzoni mwa mwezi huu, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England Rio Ferdinand ameweka wazi mikakati yake mipya katika mahojiano aliyoyafanya.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ana miaka 36 ametangaza nia ya kustaafu soka baada ya klabu ya Queens Park Rangers kutangaza kumtema kwenye kikosi chake.
na mkewe
Rio Ferdinand akiwa na marehemu mkewe Rebecca
Alitangaza uamuzi wake katika mahojiano ya moja kwa moja na BT Sport, na aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe, Rebecca aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ambaye wamezaa naye watoto watatu.
Ferdinand hakuacha kumsifia kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni mfano wa kuigwa kutokana na ujuzi wake.
Manchester United ilitoa Pauni Milioni 30 kumnunua Ferdinand Julai mwaka 2002 na kumfanya awe beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United.

Related Posts:

  • MANCHESTER UNITED YARUDI TENA KWA JORGE MENDES Hali inazidi kuchafuka barani ulaya,ndege zinazidi kupishana hii inatoka huku nyingine inatoka kule kwaajili ya kukamilisha jambo. Sasa kuna habari imetoka kwamba uongozi wa United wameamua kumwendea JORGE MENDES wakala wa R… Read More
  • WENGER "YUKO MACHO" KUTAFUTA MSHAMBULIAJI Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kununua mshambuliaji mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu. Huku mshambuliaji wao Olivier Giroud akiwa majeruhi, Arsenal walilazimishwa sare ya 1-1 na Leicester iliyopanda… Read More
  • Falcao akubali kutua Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu.Taarifa tulioipata BantuTz SPORTS hivi punde ni kwamba mshambuliaji hatari kutoka Klabu ya AS Monaco ya Ufaransa amekubali kujiunga na Manchester United kwa mkopo wa Muda mrefu huku akiwa anapokea mshahara unaokadiriwa kuwa P… Read More
  • Chicharito ajiunga Real MadridChicharito amejiunga rasmi na klabu ya nchini spain Real Madrid kwa mkopo wa mwaka mmoja na chaguo la kuuzwa moja kwa moja mwisho wa msimu kwa dau la paundi milion 22 … Read More
  • ARSENAL YAJITOA KUMUWANIA REMYKlabu ya Arsenal imejitoa ghafla katika mbio za kuifukuzia saini ya mshambuliaji wa QPR Mfaransa Loic Remy masaa machache baada ya kudaiwa kuwa imerudi kumuwania tena siku ya jana. Sasa milango iko wazi kwa nyota huyo kutua C… Read More

0 comments:

Post a Comment