Facebook

Monday 25 May 2015

ARTETA FITI KUIKABILA ASTON VILLA

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema nahodha wake, Mikel
Arteta ambaye hajacheza toka Novemba mwaka jana kwasababu ya
majeruhi anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe
la FA dhidi ya Aston Villa utakaofanyika Jumamosi hii.
Akihojiwa Wenger amesema uwezekano wa kumtumia Arteta katika
mchezo huo ni mkubwa kwasababu yuko fiti na amekuwa akifanya
mazoezi na wenzake.
Kocha huyo aliongeza kuwa beki wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu
Debuchy pia ana nafasi ya kuwepo katika kikosi chake lakini
mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Danny Welbeck hatakuwa
fiti kwa ajili ya mchezo huo.
Wenger pia amepata ahueni baada ya nyota wake Jack Wilshere na
Theo Walcott kuonyesha kurejesha makali yao kwa kucheza kwa
kiwango cha juu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya West
Bromwich Albion ambao walishinda mabao 4-1.

0 comments:

Post a Comment