Facebook

Saturday 30 May 2015

TETESI ZOTE ZA USAJILI WA WACHEZAJI BARANI ULAYA.

Mchezaji Paul Pogba anawindwa na klabu kubwa barani ulaya zikiwamo Manchester united ,Real Madrid, Manchester City, Chelsea na PSG.
Wakala wake Mino Raiola amesema anapokea simu nyingi za ofa ya mteja wake kiungo Mfaransa Paul Pogba mwenye miaka 22 anayekipiga Juventus ya Italia.Lakini amesema mteja wake kwa sasa ameelekeza nguvu zake katika mchezo wa fainali ya Ulaya utakaochezwa June 6 mapema mwezi ujao dhidi ya Barcelona.Thamani ya Pogba kwa sasa ni Euro milioni 80. 

CASSILAS AMKARIBISHA DE GEA REAL MADRID
 

Kipa wa Real Madrid Iker Casillas amesisitiza kumkaribisha kipa wa Manchester United David de Gea na amesema haogopi ushindani katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kipa De Gea anahusishwa na mipango ya kuhamia La Liga msimu ujao.
Nafasi ya Casillas katika timu hiyo ni kipa chaguo la kwanza, atakuwa katika ushindani wa hali ya juu kama De Gea atahamia klabuni hapo. Hata hivyo kipa huyo mzoefu amesema ‘kama De Gea anakuja, namkaribisha sana '
Na ameongeza 'mashindano ni afya na katika mkataba wangu hakuna kipengere kinachonitaka kuwa kipa namba moja,tutashindana kama tunavyofanya katika timu ya taifa.'Amemaliza Casillas.Je!De Gea ataweza vita ya kugombania namba na mkongwe Casillas?


 FALCAO MBIONI KUJIUNGA LIVERPOOL
Liverpool FC Tanzania's photo.
Baada ya msimu mbaya pale Old Trafford Mchezaji wa zamani wa Monaco raia wa Colombia Rademel Falcao anahusishwa na mipango ya kuhamia timu za Liverpool, Atletico Madrid, Chelsea, na PSG
Majeruhi yanatajwa kuwa chanzo cha kushusha kiwango cha mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa ada ya Euro milioni 43, sasa thamani yake inaelezwa kuwa ni Euro milioni15.
Falcao mwenye miaka 29, anatajwa kujiunga na Liverpool msimu ujao kama sehemu inayoweza kuwa na furaha kwake.Je! anaweza kuwa kuvaa viatu vya washambuliaji wetu waliopita kama Torres?



BENITEZ KUELEKEA REAL MADRID
 
Kocha Rafa Benitez amesema kwamba ataondoka Napoli mwisho wa msimu huu baada ya kukaa miaka miwili kama meneja wa timu hiyo.
Kocha huyo wa Hispania anatajwa kwenda timu ya Real Madrid, kuchukua nafasi ya kocha Carlo Ancelotti aliyetimuliwa Jumatatu.
Je! mzaliwa huyo wa Madrid Benitez anastahili kwa sasa kuwa kocha mpya wa timu kubwa kama ya Real Madrid.

LIVERPOOL YAMTENGEA DAU NONO BENTEKE.
 
Timu ya Liverpool ipo katika mbio za kumnasa mchezaji Christian Benteke. Lakini mchezaji huyo anataka awe chaguo la kwanza ikiwa ataondoka Aston Villa na kwenda Anfield.
Timu za Liverpool, Chelsea na Manchester United zote zinaonekana kumtolea macho mshambuliaji huyo Christian Benteke
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anahitaji acheze mechi nyingi ili asikosekane katika michuano ya kombe la Ulaya Euro 2016.
Wenyewe Aston Villa wameonyesha matamanio yao kwa wachezaji Emmanuel Adebayor na Charlie Austin kama mbadala wa Benteke akiondoka klabuni hapo.



STERLING KUHAMIA MAN CITY

Mchezaji wa Liverpool Raheem Sterling anahusishwa na kusajiliwa Manchester City msimu ujao.
Mshambuliaji wa Engand anataka kuondoka Anfield, anasema anahitaji kucheza michuano ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya, wengine wanasema ni fedha.
Mchezaji huyo mwenye thamani ya Euro milioni 50 anatajwa pia katika mbio za timu za Chelsea na Real Madrid.
Kwa aina ya uchezaji na washambuliaji wa Manchester City hivi leo Raheem ana nafasi ya kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo itakayoshiriki kombe la klabu bingwa barani Ulaya.?


CHELSEA YARUSHA NDOANO KWA FALCAO.
Chelsea Football Club Tanzania's photo.
Baada ya msimu mbaya pale Old Trafford Mchezaji wa zamani wa Monaco raia wa Colombia Rademel Falcao anahusishwa na mipango ya kuhamia timu za Liverpool, Atletico Madrid, Chelsea, na PSG. Majeruhi yanatajwa kuwa chanzo cha kushusha kiwango cha mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa ada ya Euro milioni 43, sasa thamani yake inaelezwa kuwa ni Euro milioni15 tu.

0 comments:

Post a Comment