Facebook

Friday 29 May 2015

Uchambuzi Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya: Barcelona vs Juventus Na Mr.Choi.

   Oya tusepe huo uzee wako usifanye safari ikawa ngumu tuendeleze stori na safari tuanze si unakumbuka jana tuliangazia upande wa magoli huku tuki acha watu midomo wazi baada ya baadhi kutokudhaniwa kuwa wapo katika miongoni mwa historia za magoli hasahasa mchezaji wa Swansea- Mafetimbi Gomis.

   MALDIN-Ni kweli sasa ngoja tuangazie upande wa Makocha ambapo kocha wa kwanza kutwaa Uefa ni Muhispanyola José Villalonga akiwa Real Madrid ambapo alifariki 7/8/1973.

    CHOI-Pia hapo mkongwe kumbuka Luis Carniglia ndie kocha wa kwanza nnje ya bara la ulaya kutwaa ubingwa wa Uefa 1958 akiwa Real Madrid na huyu ni raia wa Argentina.

   MALDIN- Lakini dogo kwenye muonekano mpya wa Uefa kwanzia 1992 kocha wa kwanza kulitwaa ni Raymond Goethals wa Ubelgiji akiwa na Marseille ambayo ndio timu ya kwanza kuchukua msimu huu mpya.

     CHOI- Ase kiukweli kila kipya kina wanao weka rekodi ambazo kufutika kwake wanadai hadi mwisho wa Dunia.

      MALDIN- Na ukiangazia upande wa makocha walio chukua ubingwa huu mara nyingi ni wawili tu Bob Paisley akichukuwa na Liverpool 1977,1978 na 1981 pia Carlo Ancelotti akiwa Ac Milan 2003,2007 na Real Madrid alipo timuliwa msimu huu 2014.

   CHOI- Ila pesa haina adabu wala haijui kuangazia wasifu wa mtu maana ukitizama historia ya Ancelotti na kutimuliwa kwake dah.!

   MALDIN- aaah! Huko sipo ukiachilia rekodi za hao wawili ila ni makocha watano ndio waliofanikiwa kuchukua ubingwa huu katika vilabu tofauti akiwemo mzee Ancelloti.

   CHOI- Hapo napajua ngoja nimalizie wengine ni Ernst Hapel 1970- Feyenoord , 1983-Hamburg , Ottmar Hitzfeld 1997- Dortmund, 2001 B.Munich, Mourinho 2004 -Fc Porto , 2010 Intermilan na Jupp Heynckes 1998 akiwa Real Madrid 2013 Bayern Munich.

      MALDIN- Kumbuka dogo takribani makocha 17 wamechukua ubingwa huu mara mbili na kama ulikuwa hufahamu Uingereza ndipo kombe lilitua mara nyingi zaidi mfululizo kwanzia 1977 alipo chukua Liverpool hadi
1982  alipochukua Aston Villa ni mara 6 katika vilabu vitatu tofauti Liverpool,Notigham foresta na Aston Villa .

   CHOI-Oya mkongwe naanza kuchoka hii safari ni noma ngoja nimalize engo ya mwisho na wewe umalizie . Unajua kwenye orodha ya makocha Taifa la Italy ndipo makocha wengi wamechukua 11 wakifuatiwa na Uhispania 9, Uingereza 7 sawa na Ujerumani dimba la tano ni Uholanzi 5 ina maana Luis Enrique na Allegri wanatafuta ubingwa kuongeza takwimu za mataifa yao.

   MALDIN - Ule mti una kivuli kizuri ngoja nimalize fasta tuka doji pale, takribani makocha 6 ndio wametwaa ubingwa huu wakiwa wachezaji na makocha yupo Miguel Munoz-Real Madrid,Giovanni Trapattoni-Ac Milan na Juventus, Johan Cruyff-Ajax na Barcelona, Ancelotti-Ac Milan, Frank Rijkaard-Ac Milan na Barcelona  kisha Guardiola ndani ya Barcelona kama mchezaji na kocha.
      
     Ndo hayo tu usisahau kutuma maoni yako kupitia

   Choikangta.ckt@gmail.com7

0 comments:

Post a Comment