Facebook

Friday 29 May 2015

Mussa Hassan Mgosi arejea Msimbazi.

SIMBA SC imemsajili tena mshambuiaji wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi(pichani)leo hii, baada ya takriban misimu miwili mizuri akiwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema leo mjini Dar es Salaam kwamba wamemrejesha Mgosi kikosini baada ya kuvutiwa na juhudi zake akiwa Mtibwa.

“Kwa Mgosi, Simba ni nyumbani kwake. Alikuwa hapa, tukamuuza DC Motema Pembe (ya DRC), akarudi, akaenda Mtibwa.

Na sisi, baada ya kuona bado ana uwezo wa kuisaidia timu yake,

Mgosi alisajiliwa na Simba SC mwaka 2005 kutoka Mtibwa Sugar namwaka 2012 akauzwa DC Motema Pembe ya DRC, ambako alicheza kwa misimu miwili.

Mwaka jana, Mgosi alirejea nyumbani baada ya kumaliza Mkataba wake Kongo na kusaini timu yake ya zamani, Mtibwa- lakini baada ya kung’ara Manungu kwa misimu miwili, amerejeshwa kundini.

Mgosi anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Simba SC ndani ya wiki moja, baada ya awali klabu hiyo kuwasajili kiungo Peter Mwalyanzi kutokaMbeya City, mabeki Samih Hajji Nuhu kutoka Azam FC na Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu.

0 comments:

Post a Comment