Facebook

Sunday 31 May 2015

Barcelona bingwa Copa Del Rey.


Timu ya Barcelona imeifunga Athletic Bilbao magoli 3 - 1 katika fainali ya Copa del Rey iliyochezwa usiku wa jana katika dimba la Nou Camp.
1 - 0 Lionel Messi alifunga goli la mapema dakika ya 20 kwa kuwapita mabeki wanne kabla ya kufunga goli murua la kukumbukwa .
2 - 0 Neymar alimalizia pasi vizuri dakika ya 36 ya mchezo na kuwaongezea vijana wa Catalans goli la pili usiku wa jana.
3 - 0 Nyota wa Argentina Messi alifunga tena kipindi cha pili dakika ya 74 goli la tatu kwa mabingwa hao wa La Liga.
3 - 1 Wageni walipata goli lao la kufutia machozi dakika ya 79 ya mchezo huo.
Barca inabaki na kibarua cha kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya dhidi ya Juventus kukamilisha vikombe vitatu msimu huu

0 comments:

Post a Comment