Facebook

Tuesday 26 May 2015

WAGONGA NYUNDO WA LONDON WAULA EUROPA

West Ham United wamefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League Msimu ujao baada ya kumaliza ligi ikiwa ni timu ya kwanza iliyocheza mchezo wa kiungwana (Fair Play).

West Ham itapaswa kuanzia hatua ya awali ya michuano hiyo hatua ambayo imebaki siku 37 tu kuanza yani wachezaji wa West Ham wanasiku chache sana za Kupumzika kabla ya kuanza michauno hiyo.

Ikumbukwe pia West Ham imempoteza kocha wake Sam Alladayse baada ya kutimuliwa na uongozi licha ya kushika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 47 sawa na Everton walioshika nafasi ya 11.

Sam alitimuliwa kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo katika mechi zake za mwisho licha yakuanza vizuri msimu uliopita.

0 comments:

Post a Comment