Facebook

Monday 25 May 2015

HUENDA VIDAL AKATUA ARSENAL

KLABU ya Arsenal, imeripotiwa kupanga muda wao kwa ajili ya
kutangaza usajili wanyota wa Juventus, Arturo Vidal.
Vidal alikuwa katika mipango ya usajili ya Manchester United
kiangazi mwaka jana lakini walikatishwa tamaa kufuatia Juventus
kutaka kitita cha paundi milioni 40.
Hata hivyo, kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni nchini
Italia, Liverpool wameambiwa kuwa wanaweza kumsajili nyota huyo wa
kimataifa wa Chile kwa paundi milioni 25.
Taarifa hizo zinachanganya zaidi baada ya mwandishi wa habari
kutoka Argentina Hernan Feler sasa kudai usajili wa Vidal kwenda
Arsenal umeshakamilika.Mwandishi huyo ambaye anaripotiwa kuwa
ndiye aliyevujisha taarifa za Arsenal kutaka kumsajili Alexis Sanchez
kutoka Barcelona msimu uliopita, aliandika katika ukurasa wake wa
twitter kuwa baada ya michuano ya Copa America klabu itatangaza
rasmi kumsajili nyota huo.

0 comments:

Post a Comment