Facebook

Monday 25 May 2015

BRENDEN RODGERS:WAMILIKI NDIO WENYE MAAMUZI JUU YANGU.

Huku Mashabiki wakipandwa na jazba kwa Timu yao kubamizwa Bao
6-1 na Stoke City hapo Jana, Meneja wao Brendan Rodgers amesema
ataondoka Liverpool ikiwa Wamiliki wake watataka hilo.
Jana huko Britannia Stadium Liverpool waliaaga Msimu wa Ligi Kuu
England kwa kichapo hicho cha Bao 6 na pia kumuaga Kepteni wao
Steven Gerrard ambae anaondoka kwenda kumalizia Soka lake huko
Marekani.
Rodgers amekiri kuwa yuko kwenye presha kubwa baada ya kushinda
Mechi 2 tu katika 9 zilizopita na kumaliza Nafasi ya 6 kwenye Ligi
ikimaanisha Msimu ujao watacheza UEFA EUROPA LIGI.
Pia Rodgers amekiri ni fedheha kwa Timu yao kupigwa Bao 6 kitu
ambacho hakijatokea kwao kwa Miaka 52 na kuwaomba radhi
Mashabiki wao.
Katika Mechi hiyo Brendan Rodgers alimpiga benchi Staa wao
Raheem Sterling ambae amegoma kusaini Mkataba mpya na
kung'ang'ania kuhama.
Hadi Mapumziko Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 5-0 zilizofungwa
ndani ya Dakika 23 na Mame Biram Diouf, Bao 2, Jonathan Walters,
Charlie Adam na Steven N'Zonzi.
Bao pekee la Liverpool lilifungwa na Steven Gerrard katika Kipindi
cha Pili ambacho pia Stoke walipiga Bao lao la 6 kupitia Peter
Crouch.

0 comments:

Post a Comment