Facebook

Thursday 28 May 2015

SEVILLA YAWEKA HISTORIA EUROPA LIGI

HATIMAYE Sevilla wameibuka mabingwa wa ligi ya Europa baada ya kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Dnipro katika mechiya fainali iliyomalizika usiku wa jana National Stadium, Warsaw.

Mapema dakika ya 7′ Dnipro waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Nikola Kalinic,lakini dakika ya 28′ Grzegorz Krychowiak akaisawazishia Sevilla.

Dakika ya 31′ Carlos Bacca akaifungia Sevilla goli la pili, lakini Ruslan Rotan akaisawazishia Dnipro dakika ya 44′.

Carlos Bacca ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kufunga goli la tatu na la ushindi kwa Sevilla katika dakika ya 73′.

    Kwa ushindi huo Sevilla imejinyakulia zawadi ya pesa kiasi cha  €5,000,000 huku washindi  wa pili  Dnipro wakipata kiasi cha  €2,500,000.
  
       Kabla ya fainali hiyo      Juventus,Internazionale,Liverpool na Sevilla zilikuwa vinara  kwa kuchukua mara 3.

       Sasa Sevilla ndio mabingwa wa kihistoria kwa kuchukua  kombe hili mara 4  kwa miaka ya 2006, 2007 2014 na 2015 .

0 comments:

Post a Comment