Facebook

Thursday 28 May 2015

SIMBA YAJIBU MAPIGO YASAJILI WAWILI:

SIMBA SC imesajili mabeki wawili wa Kizanzibari, Samir Hajji Nuhu wa kushoto na Mohammed Fakhi wa kati usiku wa leo.

Nuhu alikuwa mchezaji wa Azam FC kwa misimu miwili hadi msimu wa 2013/2014 kabla ya kuumia goti nakuondolewa katika usajili, wakati Fakhi msimu huu amechezea JKT Ruvu.

Mabeki hao vijana wadogo wamesaini leo mikataba ya kuitumikia Simba SC, Nuhu mwakammoja na Fakhi miaka miwili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema usiku huu kwamba wanatarajiwa mambo mazuri kutoka kwa wachezaji hao vijana wadogo.

“Huyu Nuhu kwa wenye kumkumbuka alipokuwa AzamFC kabla ya kuumia. Na yeye ndiye aliyekuwa beki chaguo la kwanza upande wa kushoto.

Lakini baada ya kupitia vipimo vyake na kujiridhisha kwamba amepona kabisa, tumempa nafasi nyingine,”amesema Poppe.

Aidha amesema Fakhi alikuwa beki tegemeo wa kati wa JKT Ruvu msimu huu na wengi walivutiwa na ukabaji wake mzuri.

“Mimi binafasi niseme ni mmoja kati ya watu waliopendezewa na ukabaji wa huyu kijana. Lakini si hivyo, kama utakumbuka mechi yetu ya mwisho  ya Ligi tulicheza na JKT Ruvu, hivyo baada ya mechi hata benchi laUfundi lilimpendekeza huyu mchezaji,”amesema.

Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika watatu baada ya mwanzoni mwa wiki kusajiliwa kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi.Simba SC imekuwa na bahati ya kuwasajili wachezaji wote hao wote wakiwa huru baada ya kumaliza mikataba yao katika klabu zao.

0 comments:

Post a Comment