Facebook

Saturday 30 May 2015

Kuelekea fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya hiki ndicho alichosema Lionel Messi.

.
Lionel Messi amesema timu ya Juventus si rahisi kuishinda lakini Barcelona ipo tayari kushindana.
Mkali Messi anakubali kwamba lolote linaweza kutokea katika mchezo huo ambao utachezwa mwishoni mwa wiki ijayo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Nae mshambuliaji wa Juventus Carlos Tevez amesema wao watashambulia muda wote kudhihirisha ubora wao.
Barca ni timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo katika fainali itakayochezwa mjini Berlin.
Juventus inacheza fainali hii kwa mara ya kwanza tangu icheze mwaka 2003, lakini si timu ya kuibeza.

0 comments:

Post a Comment