Facebook

Wednesday 27 May 2015

MOURINHO ABWAGWA TUZO ZA MAKOCHA:


Kocha wa timu ya soka Bournemouth ya England Eddie Howe ametajwa kuwa meneja bora wa mwaka wa shirikisho la mameneja wa soka nchini Uingereza LMA.
Kutajwa kwa meneja huyo kunakuja kufuatia kuiongoza kwa mafanikio klabu yake ambayo imeingia ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza tokea ianzishwe zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Howe anakuwa kocha wa nne kutoka nje ya ligi kuu kushinda tuzo hiyo tangia mwaka 1992 waliochukua kabla yake -1996- Peter Reid- Sunderland, 1997- Danny Wilson-Barnsley na 2006 -Steve Coppell- Reading
"siamini kabisa, ni jambo ambalo nisilotarajia" alisema kocha huyo alie mbwaga kocha bora wa msimu ligi kuu Jose Mourinho.

0 comments:

Post a Comment