Facebook

Thursday 21 May 2015

Mtibwa yamnasa kocha mpya,Mexime hatiani.

KOCHA Mbelgiji Piet de Mol aliyekuwa anawania kurithi mikoba ya Goran, amewasili leo Dar es Salaam na kwenda kukaa meza moja na Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser.

Mtibwa walimtumia usafiri de Mol Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, ambao ulimpeleka kwenye ofisi za Mratibuwake, Jamal Bayser, barabara ya Nyerere.

Mara moja Mtibwa wakafanya mazungumzo na kocha huyo na taarifa za awalizinasema wamemalizana, kilichobaki ni klabu huyo bingwa ya zamani nchini yenye maskani yake, Turiani, Morogoro kutangaza ndoa hiyo na Mbelgiji huyo.

   Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 60 ambaye ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya anaweza kuwa bosi wa kocha Mkuu wa sasa Mtibwa, Mecky Mexime.

Mwaka jana, Piet de Mol alikuwa nchini Ghana akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi Mbali na Ghana ambako alifanya kazi na Asante Kotoko, De Mol amefundisha timu pia kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China.

Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.Ilibaki kidogo Mbelgiji huyo arithi mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic klabu ya Simba SC ambayo awali ilishindwa kufikia makubaliano ya Mkataba mpya na kocha huyo aliyetakakiwango cha fedha.Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema wiki iliyopita kwamba Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000(Sh. Milioni 16).

Lakini sasa Kopunovic, aliyeiongoza Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne, amekubali kurudi kazini Msimbazi.

NB::
        Picha ya juu akiwasili leo na picha ya chini akiwa na mratibu wa Mtibwa sugar Jamal Bayser.

0 comments:

Post a Comment