Facebook

Saturday 23 May 2015

JE NOOIJ KUTIMULIWA ?

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inarejea leo baada ya kuboronga kwenye michuano ya Kombe la COSAFA ikirejea bila ushidi, kufuatia kufungwa mechi zote, lakini kocha Mart Nooij hatafukuzwa.

Huenda Mholanzi huyo ataendelea na kazi kwa hoja moja tu ya msingi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halina fedha za kumlipa kuvunja naye Mkataba, ambao unamalizika Mei mwakani.

Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kesho Dares Salaam kujadili mwenendo wa timu zote za taifa na ajenda kubwa inatarajiwa kuwa Nooij, ambaye katika mechi 16 alizoiongoza Stars tangu awasili mwishoni mwa Aprili kuchukua mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen ameshinda tatu tu, akifungwa sita na sare sita.

0 comments:

Post a Comment