Facebook

Thursday 28 May 2015

UEFA yamshinikiza Blatter kujiuzulu.

Rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA Sepp Blatter,amekataa kata
kata kujiuzulu.
Rais wa shirikisho la soka barani ulaya Michel Platini amewambia
waandishi wa habari kuwa Blatter amekataa wito wa kujiuzulu.
Platini amesema kuwa kufuatia uamuzi huo UEFA sasa itashiriki
uchaguzi hapo kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura
mpinzani wa Blatter mwanamfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Bara la Afrika limeahidi kumpigia kura Blatter sawa na shirikisho la
bara Asia.
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter,amekataa
kata kata kujiuzulu.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 anawania nafasi ya kuwa rais wa
FIFA kwa kipindi cha tano mfululizo.
Viongozi kadhaa walikuwa wamependekeza kuhairishwa kwa uchaguzi
huo huku wengine wakimtaka ajiuzulu ilikuwepo na mwanzo mpya
katika FIFA.
Awali ,Blatter aliongoza kikao cha dharura cha wanakamati wakuu wa
shirikisho hilo huko Zurich Uswisi.
Kikao hicho kinafuatia hatua ya kukamatwa kwa maafisa 7 wakuu na
polisi huko Zurich Uswisi kwa tuhuma za ufisadi.
Blatter anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu uongozi wa FIFA.
Blatter anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu uongozi wa FIFA.
Hata hivyo FIFA inasema kuwa kura za kumchagua rais mpya
zilizoratibiwa kufanyika kesho zitaendelea mbele.
FIFA ilijipata katika mkono mbaya wa sheria baada ya maafisa wa
kitengo cha FBI kupendekeza kushtakiwa kwa maafisa wakuu 14 wa
shirikisho la soka duniani FIFA kwa tuhuma za ulaji rushwa na
ufisadi.
Aidha mdhamini mkuu wa FIFA kampuni ya VISA sasa imeonya kuwa
huenda ikalazimika kutathmini upya uhusiano baina yake na FIFA
hususan kufuatia kukamatwa kwa maafisa 7 Zurich Uswisi kwa madai
ya ufisadi.
Putin amemuunga mkono Blatter
Wadhamini wengine McDonald's, Adidas na kampuni ya kutengeza
magari ya Hyundai wamesema kuwa wanafuatilia kwa karibu sana
matukio katika shirikisho hilo.
Coca-Cola, kwa upande wake imesema kuwa matukio hayo yameathiri
kwa kiwango kikubwa mno hadhi ya mashindano ya kombe la dunia.
Hatua hiyo inafanyika baada ya kukamatwa kwa viongozi wakuu wa
shirikisho hilo hapo jana Jumatano kwa madai ya ulaji rushwa na
ubadhirifu wa fedha.
Makampuni hayo ambayo hutoa mamilioni ya dola katika ufadhili
ilikushirikishwa katika mashindano ya FIFA yanatazama kwa makini
mikakati inayoendelea ya kupambana na ufisadi ndani ya shirikisho
la soka duniani FIFA.

0 comments:

Post a Comment