Facebook

Tuesday 26 May 2015

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT 2015.

 
Kama ilivyo ada nchini  kwa wahitimu wote kidato cha sita wanatakiwa kujiunga na  Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) kwa mujibu wa sheria ili kupata mafunzo ya kijeshi.Leo hii Jeshi la Kujenga Tifa limetangaza na kutoa majina ya wahitimu wote wa kidato cha sita mwaka huu 2015 ambao watatakiwa kuanza kuripoti katika kambi husika za Mafunzo ya kijeshi (JKT) kuanzia mwezi Juni 08 2015 na mafunzo yataanza rasmi Juni 15 2015.Mafunzo hayo yatachukua muda wa miezi 3 hadi hapo mwezi Septemba 15 2015


MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA ANA WATANGAZIA VIJANA IDADI 20000 WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2015 KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA. WANATAKIWA KURIPOTI KWENYE VIKOSI VYA MAFUNZO WALIVYOPANGIWA KUANZIA TAREHE 08 JUNI 2015. MAFUNZO YATAANZA RASMI TAREHE 15 JUNI 2015 NA KUMALIZIKA TAREHE 15 SEPTEMBA 2015.
YAFUATAYO YAZINGATIWE
  1. VIJANA WANAOTAKIWA KUJIUNGA WAWE RAIA WA TANZANIA
  2. WARIPOTI WAKIWA NA VYETI HALISI VYA KUZALIWA NA KUMALIZA KIDATO CHA SITA (LEAVING CERTIFICATE).
  3. VIJANA WENYE ULEMAVU UNAOONEKANA WARIPOTI KWENYE KIKOSI CHA RUVU.
  4. WALE WENYE MATATIZO AMBAYO YATAPELEKEA KUTOKUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA SASA WAANDIKE BARUA YA MAOMBI YA KUAHIRISHA MAFUNZO KWA MKUU WA JKT WAKIAMBATISHA VIELELEZO VYA TATIZO ALILONALO. MWAWASILIANO YOTE YAFANYIKE KUTUMIA ANUANI IFUATAYO.

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA
S.L.P 1694
DAR ES SALAAM.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA



Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako

 BULOMBORA -KIGOMA  RWAMKOMA - MUSOMA  KANEMBWA
     
 MSANGE - TABORA  MAKUTOPORA - DODOMA  RUVU - PWANI
     
 MGAMBO - TANGA  MARAMBA - TANGA  MLALE - SONGEA
     
 MAFINGA - IRINGA  MTABILA - KIGOMA






















Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa habari,makala,uchambuzi na taarifa zote kwa wakati na muda muafaka.

1 comments: