Facebook

Thursday 21 May 2015

Tanzania yakubali kipigo michuano ya COSAFA.

Mbwembwe Dimbani's photo.
TANZANIA imeaga mashindano ya Kombe la COSAFA baada ya kufungwa manao 2-0 naMadagascar katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini hapa.
Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo timu hiyo kufungwa, baada ya awali kulala 1-0 mbele ya Swaziland Jumatatu na sasa itakamilisha ratiba Ijumaa kwa kumenyanana Lesotho kabla ya kurejea nyumbani.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Duncan Lengani wa Malawi aliyesaidiwa na Arsenio Chadreque Marengula wa Msumbijina Isaskar Boois wa Namibia, Madagascar walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza mabao 2-0.
Madagascar walipata bao lao la kwanza dakika ya 13, mfungaji Rakotoharimalala Martin Njiva aliyemalizia krosiya Randriamanjaka Rinho Michel kutoka upande wa kushoto.
Randriamanjaka Rinho Michel mwenyewe akapasua ukuta wa Taifa Stars baada ya pasi ya Njakanirina Tobisoa aliyemtoka Oscar Joshua na kwenda kumtungua kipa Deo Munishi ‘Dida’.
Stars ilizidiwa kabisa uwezo naMadagascar kipindi cha kwanza na washambuliaji Juma Luizio na John Bocco hawakuwa na madhara mbeleya ukuta wa wapinzani wao hao.
Hakuna shambulizi la maana Taifa Stars walifanya kipindi hicho, wakati Dida pamoja na kutunguliwa mara mbili, lakinialiokoa mashuti kadhaa ya hatari.
Kipindi cha pili, kocha Mart Nooij alianza na mabadiliko, akimpumzisha Mrisho Ngassa na kumuingiza Simon Msuva ambaye dakika ya Dk 52 alikaribia kufunga.
Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Msuva alipokea pasi nzuri ya Said Hamisi Ndemla na kujaribu kumfunga kipa Randrianasolo Jean Dieu Gonne ambaye mpira ulimpita, lakini akawahi kugeuka na kuokoa kwa mguu.
Kocha Mholanzi, Nooij akafanya mabadiliko mengine dakika ya 55, akimtoa Ndemlana kumuingiza Shomary Kapombe.
Kuanzia dakika ya 65, Taifa Stars walianza kucheza kwa kujihami kuhofia kufungwa mabao zaidi, huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.
Nooij alimtoa Juma Luizio na kumuingiza Ibrahim Hajib dakika ya 65 na kidogo mchezaji huyo akishirikiana na Msuva waliisumbua ngiome ya Madagascar.
Razanakotho Dina alitajwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo huo.
Kumbuka Tanzania tupo nafasi ya 107 kwenye orodha ya Fifa huku Madagascar ikiwa ya 150 na Swaziland walio ifunga Stars mchezo wa kwanza wapo nafasi ya 176.

0 comments:

Post a Comment