Facebook

Tuesday 26 May 2015

JOHN TERRY AWA MCHEZAJI WA PILI KUCHEZA KILA DAKIKA NA KUSHINDA TAJI:


Mbwembwe Dimbani's photo.
John Terry alicheza kila dakika wakati Chelsea ikiweza kunyakua taji la Ligi Kuu.
Terry anaungana na mlinzi wa zamani Gary Pallister, Mlinzi wa zamani wa Manchester United, alifanya hivyo msimu wa 1992-93.
Nahodha wa Chelsea, John Terry amekuwa mchezaji wa pili wa ndani (mchezaji ambaye sio kipa) kuweza kucheza kila dakika katika kampeni ya timu yake kushinda Ligi Kuu ya Uingereza.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, amekuwa mchezaji wa kwanza wa Chelsea kufanya hivyo tangu Ligi Kuu ilipoanzishwa mwaka 1992.
Mlinzi huyo ambaye ameshatajwa kwenye kikosi bora cha msimu cha Ligi Kuu (PFA Team of The Year) kwa mara ya nne,‘amemtupia dongo’ (amemdhihaki) kocha wake wa zamani, Rafa Benitez.Benitez ambaye hakufikisha hata msimu pale Stamford Bridge, alidai mlinzi huyo hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki.
Mafanikio haya binafsi ya Terry yanamuunganisha moja kwa moja na Gary Pallister kama mchezaji ambaye si kipa kutokosa sekunde wakati timu yake ikishinda taji la Ligi Kuu.

0 comments:

Post a Comment