Facebook

Thursday 21 May 2015

Coutinho,Gerrard watamba katika tuzo Liverpool.


 Mbwembwe Dimbani's photo.
Mbrazil, Philippe Coutinho ametamba kwenye tuzo za Liverpool akibeba tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Liverpool.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 tu amethibitishwa kushinda tuzo hiyo inayotokana na kura za mashabiki katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika usiku wa jana ukumbi wa ECHO Arena.
Coutinho amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu mgumu kwa Liverpool, tena akiifungia timu mabao muhimu.
Mabao ya mashuti la mbali dhidi ya Bolton Wanderers katika mchezo wa Kombe la FA na Southampton katika Ligi Kuu ya England yakiwa miongoni mwa mabao yake ya kukumbukwa msimu huu pamoja na la ushindi dhidi ya Manchester City Uwanja wa Anfield.
Ameifungia timu ya Brendan Rodgers mabao manane katika mashindano yote msimu huu na kwa hakika amewavuia wengi kwa soka yake.
Rodgers alisema mapema kwamba Coutinho ana nafasi nzuri ya kuziba pengo la Luis Suarez aliyetimkia Barcelona msimu uliopita.
"Unaweza kulipa fedha zako kumuangali huyu kijana," Rodgers alisema February. "Ni mfano wa kuigwa na wachezaji wenzake katika nchi hii. Atakuwa mchezaji mkubwa dunaini miaka kadhaa ijayo. Mbwembwe Dimbani's photo.
Luis Suarez alikuwa katika kiwango hichi, kisha akacheza timu hii na kujipambanua zaidi na kwenda kuwa mchezaji mkubwa duniani na naweza kuona Coutinho anaelekea njia hiyo hiyo,"
Wakati huohuo nahodha anayeondoka Liverpool, Steven Gerrard ameshinda tuzo ya Mafanikio ya Muda Mrefu katika timu katika sherehe hizo za tuzo.
TUZO ZA LIVERPOOL NA WASHINDI WAKE 2015::
Mchezaji Bora wa Mwaka: Phillipe Coutinho
Mcheza Bora wa Kikosi cha Kwanza: Phillipe Coutinho
Bao Bora la Mwaka: Phillipe Coutinho
Kiwango Bora cha Mwaka: Philippe Coutinho
Mchezaji Bora Chipukizi w Mwaka: Raheem Sterling
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Kike: Fara Williams!
Tuzo ya Bill Shankley; Chris Anders
Mashabiki Bora wa Mwaka: OLSC London
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Akademy: Joao Carlos

0 comments:

Post a Comment