Facebook

Sunday, 24 May 2015

SIMBA WAJIBU MAPIGO KWA YANGA BAADA YA KUMNASA KIUNGO PETER MWALYANZI KUTOKA MBEYA CITY

WAKATI Yanga SC wakisherehekea saini ya winga Deus Kaseke, Simba SC nao wamefanya yao mchana huu.

Kiungo hodari mchezeshaji Peter Mwalyanzi kutoka timu ile ile, Mbeya City aliyotokea Kaseke amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Mwalyanzi moja ya viungo waliong’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu ambaye alikuwa anamchezesha vizuri Kaseke, amesaini ofisini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe, Mbezi, Dares Salaam.

Na Poppe aliyekuwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch akasema;

“Sisi tunajua wachezaji bora na Simba SC ndiyo nyumbani kwa wachezaji bora,”.

Poppe amesema kwamba Mwalyanzi ni pendekezo la kocha Mserbia, Goran Kopunovic lakini hata washauri wengine wa masuala ya kitaalamu wameridhishwa na uwezo wa mchezaji huyo.

Kwa upande wake, Mwalyanzi amesema kwamba anajisikia furaha kusaini timu hiyo kubwa, kwani ni hatua moja kubwa mbele katika maisha yake ya soka.

“Mchezaji yeyote anapokuwa anaibuka katika nchi hii, ndotozake ni siku moja kucheza timu kubwa kama hizi, na mimi nimefurahi sana kujiunga na Simba SC,”amesema.

Mwalyanzi ameongeza kwamba baada ya kusaini, anaomba ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki ili aweze kufanya vizuri.

Related Posts:

  • Schneiderlin mbioni kuondoka Southampton kwa dau la Paundi Milioni 25.KLABU ya Southampton inatarajia kutaka kitita cha paundi milioni 25 kwa ajili ya kiungo Morgan Schneiderlin mbaye anawindwa na klabu za Arsenal na Tottenham Hotspurs. Klabu hizo zinazotoka kaskazini mwa jiji la London, zote z… Read More
  • SAFARI YA INZAGHI YANUKIA AC MILAN.VYOMBO vya habari nchini Italia, vimeripoti kuwa Silvio Berlusconi amethibitisha kuwa atamtimua meneja wa AC Milan Filippo Inzaghi mwishoni mwa msimu baada ya matokeo yasiyoridhisha. Berlusconi ambaye ndiye mmiliki wa timu hi… Read More
  • De Gea mbioni kusaini mkataba mpya Man United.Tetesi zinazovuma hivi sasa ni kwamba Manchester united inategemea kumpa David De Gea mkataba mpya kwa muda miaka 4 ambao unathamini ya £250,000 kwa wiki muda wowote kuanzia hivi sasa. Leo hii amehudhuria katika hafla ya… Read More
  • Xavi kuwaaga mashabiki wa Barcelona Alhamisi.KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Hispania, Xavi anatarajia kutangaza uamuzi wake wa kuondoka Barcelona Alhamisi hii wakati akijiandaa kuhamia katika klabu ya Al Sadd ya Qatar. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akiitumik… Read More
  • Golikipa Peter Cech mbioni Arsenal.Wakati Arsene Wenger akikanusha kutaka kumsajili Petr Cech, wakala wa kipa huyo, Viktor Kolar amethibitisha kwamba Arsenal ni miongoni mwa klabu tatu ambazo mlinda mlango huyo wa Chelsea angependa kujiunga. Kolar amesema klab… Read More

0 comments:

Post a Comment