Facebook

Saturday 23 May 2015

Huyu ndiye 'Super Frankie Lampard.

   Baada ya kufunga pazia la Steven  Gerrard katika msimu wake wa mwisho ligi kuu nchini Uingereza sasa ni zamu ya kukunja pazia la chumba cha pili pale Etihad.

    Frank James Lampard ni  mzaliwa wa Romford-London tarehe 20/7/1978 amezaliwa katika familia ya mpira ukiachilia mbali Baba yake ambae alikuwa ni mchezaji na kocha msaidizi wa zamani wa West Ham pia ni mjomba wa Harry Redknapp miongoni mwa makocha bora wa Uingereza kwa maana hiyo ni ndugu wa mchezaji ambae kwa sasa ni mchambuzi wa soka Jamie Redknapp.

     Alianza maisha ya soka katika viunga vya London kwa wagonga nyundo West Ham mwaka 1994 na 1995 ndipo alipandishwa daraja lakin mara baada ya kupanda daraja alipelekwa kwa mkopo kunako timu ya Swansea ambapo alidumu hadi 1996 na alicheza takribani michezo tisa na kufunga goli moja ambalo ndilo la kwanza kwenye maisha yake ya soka la kulipwa dhidi ya Brighton & Hove Albion.

   Baada ya hapo alirejea London kukipiga West Ham wakati huo ikifundishwa na mjomba wake huku Baba yake akiwa kocha msaidizi.

       Tarehe 31/01/1996 ndiyo siku aliocheza mchezo wake wa kwanza kwa West Ham dhidi ya Coventry City akiingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya John Moncur, mchezo wake wa kwanza kuanza katika kikosi cha kwanza ilikuwa msimu wa 1996-1997 ilikuwa dhidi ya Arsenal tarehe 17/8/1996 na alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 16.

   Uzuri wa kujielewa kama mchezaji pindi ukipata nafasi sharti ujue kuitumie ili uzidishe ushawishi wa kupangwa mara kwa mara na ndicho alicho kifanya Lampard licha ya baadhi ya mashabiki wa West Ham kutokumkubali na hata kufikiria kuikacha timu hiyo.

   Kwenye msimu wa 1997-1998 Lampard alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 42 katika mashindano yote na kufunga jumla ya magoli 9 kwa namna hiyo takwimu za idadi ya mechi ziliongezeka kwa upande wake.

     Msimu wa 1999-2000 alicheza mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya barani Ulaya kwenye kombe la Intertoto ambapo West Ham waliwakabili Fc Jokerit na alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza dhidi Nk Osijek 16/9/1999 mwanzo mzuri wake ukazidi ongezeka kwa kushika nafasi ya tatu kwenye ufungaji wa timu akiwa na magoli 14 nyuma ya Paulo Wanchope na Pauolo Di Canio
       Pia ndo msimu alio kipiga kwa mara ya kwanza na jezi ya timu ya Taifa ilikuwa dhidi ya Ubelgiji tarehe 10/10/1999.

     Msimu wa 2000-2001 ulikuwa ni msimu wenye changamoto sana kwa klabu ya West Ham hasa baada ya kutokufanya vyema na kupelekea kocha Harry Redknapp kuikacha baada  ya kuwa nayo kwa miaka saba baada ya hatua hiyo kocha msaidizi wa ambae ni shemeji wa Redknapp Baba wa Lampard nae akaikacha timu hiyo.
     Kitu kilicho pelekea maisha ya soka ya Frank kuwa na wakati mgumu ndipo alipo hitaji kuikacha timu hiyo alio ichezea michezo 148  na kufanikiwa kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi millioni 11.

    Tarehe 19/08/2001 alicheza mchezo wake wa kwanza kwa Chelsea ilikuwa dhidi ya Newcastle United mchezo ambao timu hizo zilitoshana sare ya 1-1 pia kwenye msimu huo tukashuhudia kadi nyekundu ya kwanza ya Lampard katika mchezo dhidi ya Tottenham 16/9/2001.

    Unaweza sema ni kheri kwa wanafamilia wake kuondoka pale West Ham kitu kilicho leta ushawishi wa yeye kuondoka na kutua darajani ambapo ndipo kuna historia kubwa ya maisha yake soka ukijaribu kuangaza wapo wanao jua Lampard ni zao la Chelsea kumbe ni zao la West Ham na hii inatokana na heshima na jina kujengeka sana viunga vya Stamford Bridge.

     Kwa kuangazia wapo viungo wengi sana wa kati walio cheza ligi kuu Uingereza tangu msimu wa 1992 ila unapo mzungumzia Lampard ni kiungo mkamilifu wa kariba ya kisasa mwenye uwezo wa kucheza dimba la chini na juu si hilo tu kwani amekuwa hodari katika kufunga na ndipo unapoona utofauti wake.



    Ubora wake ndani ya uwanja umempelekea kuwa kiungo mwenye magoli mengi zaidi kwenye historia ya ligi kuu huku akishika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote ligi kuu achilia mbali kuwa yeye ni mfungaji wa muda wote ndani ya klabu ya Chelsea.

   Unapo zungumzia viungo hatari nnje ya 18 katika kupiga mashuti huwezi muacha Lampard na moja ya goli zuri ni msimu wa 2005 mchezo dhidi ya Crystal Palace alipo funga goli takribani yadi 30.

     Alifunga magoli matatu  kwenye mchezo mmoja kwa  mara ya kwanza ktk mechi   dhidi ya Macclesfield town msimu wa 2007  na moja ya magoli kivutio ya Lampard ilikuwa msimu wa 2008 dhidi ya Hull city achilia mbali goli bora dhidi ya Barcelona kwenye hatua ya makundi pale Camp Nou msimu wa 2006-2007 kwa kufunga goli katika moja ya engo ngumu.

       TURUDI NYUMBANI

   " Huu ni ukweli vya wenzetu vimepangilika na unaona kabisa shabaha ya mchezaji ni ipi unaona lengo tofauti na sisi tunakurupuka usingizini pakiwa pamekucha matokeo yake tunawasha tochi mchana tunafanya vitu kwa mazoea pasipo huitaji wa kujifunza zaidi lazima wachezaji wetu waige mifano mizuri ndani ya uwanja."

   Si magoli tu bali hata kutengeneza kwa wachezaji wenzake Lampard anashika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wachezaji wanao ongoza kutoa pasi za mwisho za magoli kwenye ligi kuu ya Uingereza.
    
   Mafanikio binafsi kapata mengi sana kubwa kabisa ni kushika nafasi ya pili kwenye tuzo za mchezaji bora wa Dunia  (Ballon d'Or ) msimu wa 2005 akiwa ni mchezaji wa kwanza wa Chelsea kupata mafanikio hayo na miongoni mwa wachezaji wachache wa Uingereza kufika hatua hiyo

     Vilevile upande wa makombe kachukua mengi ila kwa ngazi ya juu kachukua Ligi kuu mara 3, kombe la FA 4, Capital one 3, Ngao ya jamii 2, Mabingwa Ulaya 1 na Europa ligi 1.
 
     Kumbuka yote haya ni ndani ya Chelsea kabla ya kuikacha baada ya kuisha mkataba wake 2013 na kuwa huru kisha kutimkia New York City Fc baadae kuja Manchester City kwa mkopo

   Ni mafanikio makubwa kwa ngazi ya kilabu wapo wachezaji wengi walio cheza kwa viwango vikubwa ila upande wa kunyanyua makwapa ugumu ukawepo heshima kubwa na mafanikio yake ndani ya Chelsea yatabaki kukumbukwa ingawa mchezo wa Chelsea dhidi ya Manchester City  tarehe 21/9/2014 kidogo ulimuweka doa mbele ya mashabiki wa Chelsea baada ya kuwasawazishia Manchester City ila bado atabaki nuru angaza kwa vizazi vya wachezaji watakao kipiga darajani.

    Ingerikuwa ni maswala ya uongozi basi tunge muita msaliti wa Taifa lake ila kwa kuwa ni mpira na moja ya sifa yake ni mchezaji kutimiza majukumu yake ndani ya uwanja basi haikuwa na haja kumlaumu.

    Pale Uingereza walihesabika  viungo wawili Lampard na Gerrard kuwai kutokea katika kizazi chao kitu ambacho pia kuna mda kili leta ugumu wa kuchezeshwa pamoja timu ya Taifa kutokana na ufanano wao.
     Wote wanaikacha Ligi yenye mvuto Duniani na kutimkia Marekani.

    Vipo vingi sana vya kumuangazia Frank Lampard kiungo mfano wa kuigwa ndani ya uwanja,upande mwingine kumbuka ni kisababishi cha kutumia teknolojia ndani ya uwanja kwenye upande wa kuamua kama mpira umeingia ndani ya mstari wa goli au hauja ingia katika magoli yenye utata na hili lilichagizwa na shuti lake kwenye kombe la Dunia 2010 kwenye mchezo dhidi ya Ujerumani baada ya mwamuzi kukataa goli ambalo alidai mpira haukuvuka mstari ila kupitia marudio ya video ikaonekana ni goli.

    Huyo ndo Lampard ambae pengine kuondoka kwake hakujawa na msisimko mkubwa kama kwa Gerrard mzalendo wa ukweli

     Tumefunga pazia la Gerrard na Lampard kwenye ligi kuu nchini Uingereza historia zao, ufundi wao utabaki vichwani mwa wanasoka.

KWA MAONI:
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment